Kaimu Mkurugenzi Msaidizi
Idara ya Uendelezaji Maeneo ya Malisho na Rasilimali za vyakula vya Mifugo
(WMUV), Bw. Rodgers Shengoto akitoa maelezo mafupi kwa Mgeni Rasmi kuhusu mada
zilizowasilishwa katika mafunzo hayo ya siku mbili ya wakaguzi wa vyakula vya
Mifugo kwa Kanda ya Mashariki na Kati, yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo
Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) mkoani Morogoro. (23.10.2020)
Washiriki wa mafunzo ya
ukaguzi wa vyakula vya Mifugo wakisikiliza kwa makini mgeni rasmi ambaye pia ni
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo
pichani) wakati akifunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu
cha Kilimo Sokoine (SUA), mkoani Morogoro. (23.10.2020)
Mkurugenzi wa Idara ya
Uendelezaji Maeneo ya Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo (WMUV), Dkt.
Asimwe Rwiguza akitoa taarifa fupi kwa mgeni rasmi kuhusu mafunzo ya siku mbili
ya wakaguzi wa Vyakula vya Mifugo wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika
katika ukumbi wa Chuo cha Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) mkoani Morogoro.
(23.10.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa hotuba ya kufunga mafunzo
ya siku mbili ya wakaguzi wa vyakula vya Mifugo Kanda za Mashariki na Kati,
yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA) mkoani Morogoro.
(23.10.2020)
Mshiriki wa mafunzo ya siku
mbili ya wakaguzi wa vyakula vya Mifugo Kanda ya Mashariki na Kati, Bi. Odetha
Mchunguzi akitoa neno la shukrani kwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya wenzake, wakati
wa ufungaji wa mafunzo hayo, yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kilimo
Sokoine (SUA) mkoani Mororgoro. (23.10.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akimvalisha kitambulisho mmoja wa
wahitimu wa mafunzo ya siku mbili ya wakaguzi wa Vyakula vya Mifugo kwa Kanda
ya Mashariki na Kati yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kilimo
Sokoine (SUA) mkoani Morogoro. (23.10.2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni