Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) akikabidhi Injini ya Boti kwa
Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Wavuvi Zilagula, Bi. Agness Mbasha
katika hafla fupi ya kugawa Injini za Boti kwa Vyama vya Ushirika vya Wavuvi
Kanda ya Ziwa Victoria iliyofanyika katika Wilaya ya Muleba, Mkoani Kagera. (23.10.2020)
Pichani ni Injini za Boti (4)
aina ya Yamaha ambazo Wizara ya Mifugo na Uvuvi imezikabidhi kwa Vyama vinne (4)
vya Ushirika vya Wavuvi Kanda ya Ziwa Victoria katika hafla fupi iliyofanyika
Wilayani Muleba, Mkoani Kagera. (23.10.2020)
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) akijadiliana jambo na
Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utafiti na Mafunzo ya Uvuvi, Dkt. Erastus Mosha (kushoto)
muda mfupi kabla ya kukabidhi Injini za Boti kwa Vyama vya Ushirika vya Wavuvi
Kanda ya Ziwa Victoria katika hafla fupi iliyofanyika Wilayani Muleba, Mkoani
Kagera. (23.10.2020)
Mkurugenzi Msaidizi, Kitengo
cha Huduma za Ugani za Uvuvi, Anthony Dadu akifafanua jambo katika hafla fupi
ya kukabidhi Injini za Boti kwa Vyama vya Ushirika vya Wavuvi Kanda ya Ziwa
Victoria iliyofanyika Wilayani Muleba, Mkoani Kagera. (23.10.2020)
Mkazi wa Kasenyi, Ikuza, Wilayani Muleba, Mkoani Kagera, Edgar Katunzi akiuliza swali kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (hayupo pichani) katika hafla fupi ya kugawa Injini za Boti kwa Vyama vya Ushirika vya Wavuvi Kanda ya Ziwa Victoria iliyofanyika Wilayani Muleba, Mkoani Kagera. Wengine katika picha ni Sehemu ya Wananchi wanaofanya shughuli za Uvuvi Mkoani humo. (23.10.2020)
Mwakilishi wa Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Bw. Omary Mchengule akizungumza katika
hafla fupi ya kugawa Injini za Boti kwa Vyama vya Ushirika vya Wavuvi Kanda ya
Ziwa Victoria iliyofanyika Wilayani Muleba, Mkoani Kagera. Kulia kwake ni
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah na kushoto
kwake ni Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Uvuvi, Stephen Lukanga. (23.10.2020)
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (katikati waliokaa) akiwa katika picha
ya pamoja na Viongozi na Wawakilishi wa Vyama vya Ushirika vya Wavuvi Kanda ya
Ziwa Victoria muda mfupi baada ya kukabidhi Injini za Boti kwa Vyama (4) vya
Ushirika wa Wavuvi wilayani Muleba, Mkoani Kagera. Kutoka kulia waliokaa ni
Mkurugenzi Msaidizi, Kitengo cha Huduma za Ugani za Uvuvi, Anthony Dadu akifuatiwa
na Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utafiti na Mafunzo ya Uvuvi, Dkt. Erastus
Mosha. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya
Wilaya ya Muleba, Omary Mchengule akifuatiwa na Kaimu Mwenyekiti Chama cha
Ushirika cha Wavuvi Zilagula, Bi. Agness Mbasha. (23.10.2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni