Afisa Mifugo (DGLF) Bi.Theodata Salema akitoa
maelezo kuhusu aina, utengenezaji, utunzaji na matumizi ya vyakula vya Mifugo
kwa wadau waliotembelea mabanda ya Wizara na Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya
wakulima, wafugaji na Uvuvi (nanenane) yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyakabindi
mkoani Simiyu (2/8/2020).
Mdau wa Hifadhi za
Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Hatibu Issa, akitoa maelezo kwa wananchi
waliotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi (nanenane) kitaifa yanayoendelea mkoani Simiyu (2/8/2020).
Mkurugenzi wa Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt.Nazael
Madala (mwenye kofia nyeusi) akimuonesha Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
mh.Antony Mavunde (mwenye tai) aina mbalimbali za teknolojoa ya ufugaji samaki
alipotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya nanenane
kitaifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu (2/8/2020).
MOROGORO
Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa
Mwandamizi wa Uhifadhi- Utalii, TANAPA- Kanda ya Mashariki, Apaikunda
Mungure(kushoto anayemuangalia) alipotembelea banda la Hifadhi za Taifa
Tanzania (TANAPA) katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kufanyika katika
Uwanja wa Mwl. Nyerere, Mkoani Morogoro Julai 2, 2020.
Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akisaini katika kitabu cha Wageni kwenye banda la
Wizara ya Mifugo na Uvuvi alipotembelea Maonesho ya Nane Nane Kanda ya
Mashariki yanayofanyika katika Uwanja wa Mwl. Nyerere Mkoani Morogoro Julai 2,
2020.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina
akionesha kuvutiwa na Samaki aina ya Kambakochi aliyemshika alipotembelea banda
la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika katika
Uwanja wa Mwl. Nyerere Mkoani Morogoro Julai 2, 2020.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga
Mpina(kushoto) akimsikiliza Msimamizi wa Idara ya Mauzo, Kampuni ya Agricom
Afrika, Mathias Lusendamila alipotembelea banda la Kampuni ya Agricom Afrika
katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kufanyika katika Uwanja wa Mwl.
Nyerere, Mkoani Morogoro Julai 2, 2020.
ARUSHA
Afisa Mtafiti Mifugo
kutoka Wakala ya Maabara ya Vetenari Tanzania (TVLA), Bw. Deogratius
Mshanga (kulia) akitoa maelezo kwa mdau kuhusu chanjo za Mifugo zinazotolewa na Maabara
hiyo, alipotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho
ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha. (02/08/2020)
Afisa Mifugo kutoka kituo cha Taifa cha
Uhimilishaji (NAIC) Usariver Arusha, Bw.Abdallah Thabiti ( kulia) akitoa
maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na kituo hicho kwa wadau waliotembelea
mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane
yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha (02/08/2020)
Mkufunzi kutoka LITA Tengeru,
Bw. Frank Moshi (kulia) akielezea hatua za kuandaa ngozi kuanzia
zinapotoka machinjioni adi kufikia hatua ya kutengeneza bidhaa kwa watumishi wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi walipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya
nanenane yanayoendelea katika kiwanja cha Themi Mkoani Arusha (
02/08/2020)
MBEYA
Afisa Mtafiti wa
magonjwa ya mifugo Geofrey Thomasi akitoa maelezo kwa mdau jinsi ya upimaji wa
magonjwa ya mifugo kimaabara na kumjulisha juu ya uwepo wa chanjo mbalimbali za
mifugo kama chanjo ya kideli,chanjo ya kimeta na chanjo ya Chambavu(BQ) alipotembelea
kwenye mabanda ya wizara ya mifugo na uvuvi katika maonyesho ya wakulima,
wafugaji na uvuvi (nanenane) viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya tarehe 02.08.2020.
Afisa kutoka bodi
ya nyama Ephraim Chawala akitoa maelezo kwa wadau kuhusu matumizi ya vifaa vya
kisasa katika uandaaji wa nyama bora na salama walipotembelea kwenye mabanda ya
wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya kilimo, Mifugo na uvuvi (nanenane)
katika viwanja vya John Mwakangale mkoa wa Mbeya tarehe 02.08.2020.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni