Makamu wa Raisi wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu (01.08.2020) amefungua rasmi kitaifa maonyesho ya 28 ya kilimo (Nanenane) katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Katika hotuba yake ya
ufunguzi, Mhe. Makamu wa Raisi alizipongeza Wizara zote za kisekta na wadau wa
taasisi za fedha zikiwemo banki za CRDB, NBC na NMB kwa maandalizi mazuri
waliyofanya kufanikisha sherehe hizo bila kuathiriwa na muda mfupi waliokuwa
nao.
“lakini pia Mhe. Raisi
amenipa salamu zenu na anawapongeza sana kwa kazi kubwa mnayofanya ya kuwawekea
mazingira wezeshi wakulima, wafugaji na wavuvi hali inayozidi kuchochea maendeleo
makubwa ya sekta hizo. Alisema Mhe. Samia.
Aliongezea kuwa Serikali
inatambua mchango mkubwa unaotolewa na sekta ya mifugo na uvuvi kwenye pato la
Taifa ambapo kwa mwaka 2019/2020 sekta ya mifugo ilichangia pato la taifa kwa
asilimia 7.4 na kukua kwa asilimia 5 huku sekta ya uvuvi ilichangia asilimia
1.7 na kutoa ajira kwa watanzania milioni 4.5.
Lakini pia katika kuhakikisha
nchi inaondokana na tatizo la upungufu wa lishe, Sekta ya Mifugo imechangia
takribani asilimia 30 katika lishe inayotokana na wanyama hapa nchini.
Alisisitiza Mhe. Samia
Akizungumzia upande wa
mchango wa dawati, Mhe. Samia alizipongeza taasisi za fedha zinazoendelea kutoa
mikopo kwa wakulima na wafugaji ikiwemo benki ya wakulima (TADB) ambayo
iliidhinisha kiasi cha bilioni 26 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wafugaji,
wazalishaji wa maziwa, wavuvi na wakuzaji viumbe maji.
Aidha benki ya posta Tanzania imefungua dirisha la mikopo kwa wavuvi lakini huku shirika la Bima la Taifa (NIC) likianzisha huduma ya bima ya mifugo ambayo kwa kiasi kikubwa itachochea ongezeko la mikopo. Aliongezea Mhe. Samia
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza
kwenye viwanja vya Nyakabindi leo (01.08.2020) muda mfupi kabla hajafungua
maonesho ya Kilimo (Nane Nane) kitaifa yanayofanyika kwenye viwanja hivyo
vilivyopo mkoani Simiyu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma muongozo wa lishe bora aliouzindua leo muda mfupi baada ya kufungua maonesho ya 28 ya Kilimo (NaneNane) katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Antony Mtaka (Kulia) na katikati mi Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel.
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (katikati) akitoa maelezo juu ya teknolojia
ya ukuzaji viumbe maji kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) wakati wa ziara yake ya kukagua mabanda ya
Sekta za mifugo na uvuvi jana (01.08.2020) kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani
Simiyu. kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof.
Elisante Ole Gabriel.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni