Mkurugenzi Msaidizi Afya ya Jamii na Pembejeo
za Mifugo (DVS) Dkt.Stanford Ndibalema akitoa maelezo kuhusu huduma bora za
afya za wanyama kwa wadau waliotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi
kwenye maonesho ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani
Simiyu (3/8/2020).
Mkufunzi kutoka Wakala ya Mafunzo ya Mifugo
(LITA), Bw. Heriel Mchome akitoa wito kupitia vyombo vya habari kwa wadau
kujiunga na mafunzo mbalimbali yanayotolewa na LITA katika kampasi zake
zilizopo mikoa nane nchini, kwenye maonesho ya nanenane yanayoendelea kwenye
viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu (3/8/2020).
Naibu Gavana wa Benki
Kuu ya Tanzania (BOT), Dkt. Bernard Kibese akihamasisha wafugaji kufika kwenye
mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kujifunza teknolojia za ufugaji wa kisasa
baada ya yeye kuvutiwa na teknolojia hizo ikiwemo mashine ya kuandalia chakula
cha mifugo na ufugaji samaki kwenye matanki.Naibu Gavana ametembelea mabanda
hayo kwenye maonesho ya nane nane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi
mkoani Simiyu (3/8/2020).
ARUSHA
Mtaalam wa Samaki
kutoka SoulPeace AquaFish Limited, Bw. Goodluck Benjamin (wa kwanza kulia)
akitoa elimu ya namna wanavyopata mayai ya kambale na utunzaji wa kambale hao
kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya
Nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha (03/08/2020)
Mchumi Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,
Dkt. Sophia Mlote (kushoto) akipata maelezo juu ya ufugaji wa sungura na faida
za mkojo wa sungura kutoka kwa mtaalam wa Sungura Bi. Renalda Chami kutoka
kampuni ya SAORE kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha
themi Mkoani Arusha. (03/08/2020)
Afisa Mifugo kutoka
kituo cha huduma za mifugo kanda ya kaskazini (ZVC), Bw. Conrad Ernest
Massawe akitoa elimu ya magonjwa ya mifugo kwa wadau waliotembelea banda la
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye
kiwanja cha Themi Mkoani Arusha (03/08/2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni