Jumatano, 29 Julai 2020
Jumanne, 28 Julai 2020
Jumatatu, 27 Julai 2020
DKT. TAMATAMAH AKISAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akisaini
kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Hayati Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu
wa Serikali ya Awamu ya Tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mara baada ya
kuhudhuria ibada ya misa takatifu ya kumuombea Hayati Mkapa katika uwanja wa
uhuru jijini Dar es Salaam. (26.07.2020)
Jumapili, 26 Julai 2020
BODI YATAKIWA KUWA BUNIFU KUBORESHA HUDUMA ZA LITA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof.
Elisante Ole Gabriel ameitaka Bodi Mpya ya Ushauri ya Wakala ya Vyuo vya Mifugo
(LITA) kuwa bunifu ili kuboresha huduma na kuleta tofauti katika shughuli zao
na kufikia malengo yake.
Prof. Ole Gabriel aliyasema hayo alipokuwa akifungua kikao kazi
cha kwanza cha Bodi mpya ya ushauri ya LITA kilichofanyika jijini Dar es Salaam
Julai 25, 2020.
Akizungumza katika kikao hicho, Prof. Gabriel aliwahimiza
wajumbe wa bodi hiyo kutumia vyema taaluma zao na kuwa wabunifu katika
kuhakikisha LITA inaboresha huduma zake na kuleta mabadiliko chanya ya
kiutendaji ya Wakala hiyo.
"Nawaomba bodi mfanye kazi yenu vizuri na mfanye
maboresho kadri itakavyowezekana, shirikianeni kwa ukaribu na wadau wengine ili
kusaidia kuboresha shughuli zenu," alisema Prof. Gabriel.
Sambamba na hilo, Prof. Gabriel ameitaka bodi hiyo
kuhakikisha inasimamia vyema rasilimali fedha za taasisi hiyo huku akiwaeleza
kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina wakati wote amekuwa mkali na
watu ambao wamekuwa wanatumia vibaya rasilimali za umma.
Aliendelea kueleza kuwa LITA wanaweze kufanikiwa katika
shughuli zao endapo wataweka mikakati ya kuboresha eneo la masoko na habari
ambalo litasaidia kutangaza na kuhamasisha jamii kupitia vyombo vya habari
kutumia huduma zinazotolewa na LITA na kwa njia hiyo wataongeza mapato.
"Hii ni taasisi ya biashara hivyo ni muhimu kuitangaza
vya kutosha ili watu waijue LITA ni nini, ipo wapi na inafanya nini, kwa
kufanya hivyo kutaivuta jamii kutumia huduma zenu," alifafanua Prof.
Gabriel.
"Serikali inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
imefanya kazi kubwa mpaka sasa tumeingia katika uchumi wa kati, hivyo LITA ni
lazima muhakikishe mnaenda sambamba na kasi hii ya uchumi wa kati kwa kuboresha
huduma zenu ikiwemo kubuni vyanzo vingine vya mapato," aliongeza Prof.
Gabriel.
Akiongea mapema katika kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Wakala ya Vyuo vya Mifugo (LITA), Dkt.
Pius Mwambene alisema kuwa mpaka sasa taasisi hiyo imepata mafanikio kadhaa
ikiwemo kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi kutoka 798 mwaka 2012/13 hadi
kufikia 3642 mwaka 2019/2020 huku akisema kuwa wameshaongeza Kampasi nyingine
mbili ambazo ni Mabuki, Mwanza na Kikulula, Kagera.
"Kuanzia Mwaka jana tumeanza kutoa gawio katika mfuko
mkuu wa Serikali ambapo tulianza kutoa kiasi cha shilingi milioni 50 mwaka jana
na mwaka huu tumetoa milioni 100,"alifafanua Dkt. Mwambene
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya LITA, Prof. Malongo Mlozi alisema
kuwa kufuatia kauli hiyo ya Katibu Mkuu watahakikisha kuwa wataweka utaratibu
kwa kushirikiana na Menejimenti kuangalia mapato na matumizi ya fedha kila
miezi mitatu, huku akieleza kuwa kwa nafasi yao wataendelea kutoa ushauri juu
ya matumizi bora ya rasilimali umma.
Kuhusu suala la ubunifu alisema kuwa wataweka mipango mizuri
kuhakikisha taasisi hiyo kupitia Kampasi zake inajiendesha kibiashara ili
kujiongezea kipato.
Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya
Wakala ya Vyuo vya Mifugo (LITA), Bi. Josephine Matiro akipitia Makabrasha
katika kikao cha kwanza cha bodi hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam. (25.07.2020)
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati waliokaa) akiwa
katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala ya Vyuo vya
Mifugo (LITA) muda mfupi baada ya kufungua kikao chao cha kwanza kilichofanyika
jijini Dar es Salaam. Kulia (waliokaa) ni Mwenyekiti wa Bodi ya LITA, Prof.
Malongo Mlozi na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LlTA, Dkt. Pius
Mwambene. Waliosimama kutoka kulia ni wajumbe wa Bodi hiyo, wa kwanza ni Dkt.
Angello Mwilawa, wa pili ni Bi. Josephine Matiro, katikati ni Prof. Zacharia
Masanyiwa. Kutoka kushoto (wa kwanza) ni Bw. Mark Tsoso na wa pili ni Bi.
Faraja Makafu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akifurahia jambo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Vyuo vya Mifugo (LITA), Dkt. Pius Mwambene muda mfupi baada ya kufungua kikao cha kwanza cha Bodi ya Ushauri ya LITA kilichofanyika jijini Dar es Salaam (25.07.2020)
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akiteta jambo na
Kaimu Mkurugenzi wa Wakala ya Vyuo vya Mifugo (LITA), Dkt. Pius Mwambene katika
kikao cha kwanza cha Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya LITA kilichofanyika jijini Dar
es Salaam. (25.07.2020)
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala ya Vyuo vya Mifugo (LITA), Prof. Malongo Mlozi (aliyesimama) akiongea na Wajumbe wa bodi hiyo wakati alipokuwa akiongoza kikao chao cha kwanza kilichofanyika jijini Dar es Salaam. (25.07.2020)
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na Wajumbe wa
Bodi Mpya ya Ushauri ya Wakala ya Vyuo vya Mifugo (LITA) wakati akifungua kikao
cha kwanza cha bodi hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam. (25.07.2020)
Ijumaa, 24 Julai 2020
MAKATIBU WAKUU WAKUTANA KUJADILI MAANDALIZI YA NANE NANE 2020
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw.
Gerald Kusaya leo (24.07.2020) ameongoza kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za
kisekta kujadili maandalizi ya Maonesho ya Kilimo Nane nane yatakayofanyika
kitaifa mkoani Simiyu kuanzia tarehe 01 Agosti, 2020.
Katika kikao hicho, Bw. Kusaya alieleza kuwa ni matarajio ya wizara ya kilimo
na zile za kisekta kuona maonesho ya Nane nane mwaka huu yanakuwa tofauti
katika kuleta mapinduzi ya, ufugaji na uvuvi ili wananchi wapate kuongeza tija
na ufanisi kukuza uchumi wa kaya na taifa.
Kikao hicho kimehusisha Makatibu
Wakuu ambao ni Prof. Riziki Shemdoe (Viwanda na Biashara), Prof. Elisante Ole
Gabriel (Mifugo), Mhandisi Anthony Sanga (Maji) na Dkt. Rashid Tamatamah
(Uvuvi) na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Miriam Mmbaga pamoja na kamati ya
maandalizi.
“Tunapenda kuona maonesho ya Nane
nane mwaka huu yanakuwa tofauti na yaliyopita katika kuwafanya wakulima, wafugaji
na wavuvi wabadilike kutoka katika kilimo cha kujikimu kuwa kilimo, ufaguji na
uvuvi wa kibiashara kupitia elimu na
teknolojia bora watakayojifunza kutoka kwa wataalam “ alisema Kusaya.
Kikao kimezishauri Wizara, taasisi na
wadau wa maonesho ya mwaka huu kujikita katika kuwasaidia wakulima,wavuvi na
wafugaji kuongeza tija katika shuguli zao ili baada ya maonesho maisha yao yawe
bora zaidi kiuchumi.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu (Mifugo)
Prof. Elisante Ole Gabriel alisema wakulima wanahitaji elimu ya kubadilisha
mtizamo hivyo matumizi ya vyombo vya habari kufikisha elimu kwa wakulima, wafugaji
na wavuvi ni muhimu sana kwenye maonesho haya.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara, Prof. Riziki Shemdoe alisema ni vema kamati ya uratibu ikaweka
utaratibu wa kuwakutanisha wafanyabiashara za mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi
pamoja na wakulima kwenye maonesho hayo hususan Simiyu.
“Tuandae maeneo kwa ajili wa
wafanyabiashara na wakulima, wafugaji na wavuvi kufanyia mazungumzo ya kukuza
upatikanaji wa masoko na kutumia fursa za biashara ikiwemo kuwekeza katika
viwanda” alisisitiza Prof. Shemdoe.
Maonesho ya Kilimo Nane nane mwaka
huu yana kauli mbiu isemayo “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua
Viongozi Bora 2020”.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ol Gabriel akizungumza
katika kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za kisekta kuhusu maandalizi ya
maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu. Kikao kimefanyika
katika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo. (24.07.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Kusaya
akiongoza kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara za kisekta kuhusu maandalizi ya
maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu. Kikao
kimefanyika katika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo. ( 24.07.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi),
Dkt. Rashid Tamatamah akizungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za
kisekta kuhusu maandalizi ya maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa
mkoani Simiyu. Kikao kimefanyika katika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa
Wizara ya Kilimo. (24.07.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.
Riziki Shemdoe akizungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za kisekta
kuhusu maandalizi ya maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani
Simiyu. Kikao kimefanyika katika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara
ya Kilimo. (24.07.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony
Sanga akizungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za kisekta kuhusu
maandalizi ya maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu.
Kikao kimefanyika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo. (24.07.2020)
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bibi Miriam Mmbaga
akizungumza kwenye kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za kisekta kuhusu
maandalizi ya ya maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani
Simiyu. Kikao kimefanyika katika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara
ya Kilimo (24.07.2020)
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia kikao cha
Makatibu Wakuu wa wa wizara za kisekta kuhusu maandalizi ya ya maonesho ya Nane
nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu. Kikao kimefanyika katika mji
wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo. ( 24.07.2020)
Alhamisi, 23 Julai 2020
WARSHA YA KAMATI YA KITAIFA YA MWONGOZO WA HIARI WA KUHAKIKISHA UVUVI MDOGO UNAKUWA ENDELEVU
Picha ya Pamoja ya baadhi ya
Washiriki wa warsha ya kutoa maoni juu ya Mwongozo wa Hiari wa kuhakikisha
Uvuvi Mdogo unakuwa endelevu iliyofanyika katika Kata ya Kilwa
Kivinje,Halmashauri ya Kilwa Masoko. (22.07.2020)
Mratibu wa Mpango wa Mwongozo
wa Hiari wa kuendeleza Uvuvi Mdogo, Bi. Lilian Ibengwe (picha ya pili kulia)
akikusanya Maoni ya wadau kwenye Warsha ya kutoa Maoni ya Wadau wa Uvuvi Mdogo
katika Kata ya Kilwa Kivinje,Halmashauri ya Kilwa Masoko. (22.07.2020)
Mdau wa Uvuvi Mdogo,
Bw.Faridu Shaweji wa Kilwa Kivinje akitoa Maoni yake leo kwenye Warsha ya
utoaji maoni kwenye Warsha ya kutoa Maoni ya Wadau wa Uvuvi Mdogo katika Kata
ya Kilwa Kivinje, Halmashauri ya Kilwa Masoko. (22.07.2020)
Mwenyekiti wa Kamati ya
Kitaifa ya Mwongozo wa Hiari wa kuhakikisha Uvuvi Mdogo unakuwa endelevu,
Bw.Yahaya Mgawe akitoa maelezo kwenye Warsha ya kutoa Maoni ya Wadau wa Uvuvi
Mdogo katika Kata ya Kilwa Kivinje, Halmashauri ya Kilwa Masoko. (22.07.2020)
Jumatano, 22 Julai 2020
ADDITION EXAMINATION NUMBERS FOR CANDIDATES EXPECTING TO SIT FOR QUALIFYING EXAMINATION.
ADDITION EXAMINATION NUMBERS FOR CANDIDATES EXPECTING TO SIT FOR QUALIFYING EXAMINATION. kupata orodha , bofya hapa
Jumanne, 21 Julai 2020
NARCO YAMSIMAMISHA KAZI MENEJA WEST KILIMANJARO
Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni
ya Ranchi ya Taifa (NARCO), Masele Mipawa amemsimamisha kazi Meneja wa Ranchi
ya West Kilimanjaro iliyopo Kilimanjaro, Hezron Kyaruzi kwa tuhuma za kukosa
uadilifu kwa mali za Umma na kusababisha upotevu wa Ng’ombe takriban 32.
Akiwa katika ziara ya
kutembelea Ranchi hiyo ya West Kilimanjaro Mipawa alisema kuwa waliamua kufanya
maamuzi hayo kufuatia changamoto nyingi zinazolikumba shamba hilo ambazo kwa
kiasi kikubwa zimechangiwa na uongozi mbovu wa meneja huyo.
“Kutokana na upotevu wa
Ngombe, uzembe na ukosefu wa maadili tumeamua kumsimamisha kazi Meneja wa
Ranchi na Msaidizi wake na hatua nyingine za kisheria na kinidhamu zitafuata ",
alisema Mipawa
Mipawa alisema ziara hiyo
aliyoifanya katika Ranchi hiyo ilikuwa na lengo la kufanya ukaguzi kutokana na
taarifa walizokuwa wakizipata ambazo zilionesha kuwa katika shamba hilo
kumetokea upotevu wa Ng’ombe ambao Kampuni ya NARCO haina taarifa nao.
Ziara hii pia imesaidia
kubaini kuwa kuna wizi uliokithiri katika shamba hili ambao umechangiwa na
mahusiano mabovu kati ya Meneja na jamii inayolizunguka shamba hilo, ukosefu wa
maadili na uadilifu wa Meneja ambao umepelekea
Ngombe 32 kupotea.
Kati ya ngombe hao 32
waliopotea 15 wameshapatikana na wengine 17 hawajapatikana mpaka sasa huku
ngombe wengine 27 walichinjwa bila kibali cha makao makuu, alifafanua Mipawa
Kufuatia hali hiyo, Mipawa
alisema wameamua pia kumsimamisha kazi Msaidizi wake kwa kuwa alishindwa
kumshauri vizuri meneja huyo huku ikidaiwa alikuwa akishirikiana na meneja huyo
kwenda kuazima ngombe kwa watu binafsi ili Ranchi hiyo ionekane ina idadi kubwa
ya ngombe.
Aidha, Mipawa aliwataka
wafanyakazi wengine waliobaki katika shamba hilo kuendelea kufanya kazi kwa
bidii, wazingatie nidhamu na uzalendo huku akiwaonya kuwa Serikali ya Awamu ya
Tano haitavumilia mtu yeyote anayehujumu rasilimali za Taifa.
Kaimu Meneja Mkuu - NARCO,
Bw. Masele Mipawa (aliyevaa suti nyeusi) akiongea na wafanyakazi wa Ranchi ya
West Kilimanjaro wakati alipokwenda kuangalia maendeleo ya ranchi hiyo.
(18.07.2020)
Kaimu Meneja Mkuu - NARCO,
Bw. Masele Mipawa akiwa amepanda farasi ambao wapo katika ranchi ya
West-Kilimanjaro wakati alipokwenda kukagua maendeleo ya ranchi hiyo.
(18.07.2020)
Kaimu Meneja Mkuu - NARCO,
Bw. Masele Mipawa akiongoza kikao cha watumishi wa Ranchi ya West-Kilimanjaro
wakati alipokwenda kukagua maendeleo ya ranchi hiyo. (18.07.2020)
Kaimu Meneja Mkuu - NARCO,
Bw. Masele Mipawa akiongoza kikao cha watumishi wa Ranchi ya West-Kilimanjaro
wakati alipokwenda kukagua maendeleo ya ranchi hiyo. (18.07.2020)
SIJARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI - DKT. TAMATAMAH.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah hajaridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa
Jeongo la Utawala la Ofisi ya Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU)
unaoendelea katika Kisiwa cha Mafia.
Dkt. Tamatamah aliyasema hayo
baada ya kukagua kazi za ujenzi zinazoendelea ambapo hakuridhishwa na kasi ya
ujenzi kwani haiendani na muda uliotumika kwa mujibu wa mkataba.
"Sijaridhishwa na kasi
ya ujenzi niliyoikuta hapa hivyo ninakuagiza mkandarasi kuhakikisha unazingatia
ratiba na muda uliopangwa kulingana na mkataba" Alisisitiza Dkt.
Tamatamah.
Jengo hilo linasimamiwa na
mkandarasi mwelekezi "Y&P architects" linatarajiwa kutumiwa na MPRU
kama ofisi mara baada ya kukamilika kwake ambapo litasaidia kuongeza ufanisi wa
taasisi hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto), baadhi ya watendaji wa sekta
ya Uvuvi na baadhi ya watendaji wa kampuni ya "Y & P Architects" wakiangalia
hatua ya ujenzi iliyofikiwa kwenye jengo la Utawala la Ofisi ya Hifadhi ya Bahari
na Maeneo Tengefu (MPRU) lililopo kwenye kisiwa cha Mafia jana (18.07.2020).
MSAJILI WA BARAZA LA VETERINARI AKAGUA BAADHI YA MADUKA YA HUDUMA ZA PEMBEJEO ZA MIFUGO - DODOMA
Msajili wa Baraza la
Veterinari Tanzania, Dkt. Bedan Masuruli akikagua moja ya Duka la utoaji huduma
za Pembejeo za Mifugo la Blessing Agrovet Techical. Kushoto ni Bi. Upendo Hamisi ambae ni mtoa huduma katika
duka hili. (17.07.2020)
Msajili wa Baraza la
Veterinari picha ya kwanza (kulia) akifunga Duka la Blessing Agrovet Technical
kwa kufuli lake. Wa kwanza kushoto ni mtoa huduma za Mifugo katika duka hilo,
Bi. Upendo Hamisi akitii amri ya kufunga duka kwa kufuli kutokana na kushindwa
kutimiza baadhi ya masharti muhimu ya utoaji huduma kwa kutokuwa na daktari wa
mifugo aliyesajiliwa na kutohuisha jina la mtoa huduma katika Baraza la
Vetenari ili awe kuwa na uhalali wa kutoa huduma. (17.07.2020)
Msajili wa Baraza la
Veterinari picha ya kwanza (kulia) akifunga Duka la Blessing Agrovet Technical
kwa kufuli lake. Wa kwanza kushoto ni mtoa huduma za Mifugo katika duka hilo,
Bi. Upendo Hamisi akitii amri ya kufunga duka kwa kufuli kutokana na kushindwa
kutimiza baadhi ya masharti muhimu ya utoaji huduma kwa kutokuwa na daktari wa
mifugo aliyesajiliwa na kutohuisha jina la mtoa huduma katika Baraza la
Vetenari ili awe kuwa na uhalali wa kutoa huduma. (17.07.2020)
Jumapili, 19 Julai 2020
ZIARA YA KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI (MIFUGO) WILAYANI KONGWA
Picha ya pamoja ya Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo, Prof. Elisante Ole Gabriel, Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt. Elligy Shirima,
uongozi wa taasisi ya PASS, pamoja na wafanyakazi wa TALIRI na vijana
wanaopatiwa mafuzo ya ufugaji bora wa mbuzi na PASS. (17.07.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyesimama) akizungumza na
wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Wilaya ya Kongwa
pamoja na vijana wanaopatiwa mafunzo ya unenepeshaji wa mbuzi na taasisi ya
PASS, ambapo amewataka kuhakikisha mafunzo hayo yanakuwa chanzo cha wao
kujiajiri na kuajiri vijana wengine kupitia ufugaji. (17.07.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (akitembelea) jengo la kituo cha
mauzo ya nyama ya mbuzi linalojengwa katika kituo cha Taasisi ya Utafiti wa
Mifugo Tanzania (TALIRI) Wilaya ya Kongwa kwa kushirikiana na taasisi ya PASS
ambayo pia inatoa mafunzo kwa vijana namna ya kunenepesha mbuzi na kufanya
biashara ya ufugaji kwa tija. (17.07.2020)
Muonekano wa shamba la
malisho ya mifugo la Bw. Mnyonaki Saileni lililopo Kijiji cha Msujile Kata ya
Sejeli Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma, ambapo Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel ameridhishwa na ubora wa malisho
hayo. (17.07.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyesimama katikati) akikagua
moja ya mbegu bora ya mbuzi alipotembelea shamba la mifugo la Bw. Mnyonaki
Saileni (wa kwanza kulia) alipofanya ziara katika shamba lake lililopo Kijiji
cha Msujile Kata ya Sejeli Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma. aliyesimama kushoto
ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt.
Elligy Shirima. (17.07.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akikagua viwele vya moja ya
ng'ombe wa Bw. Mnyonaki Saileni (hayupo pichani) baada ya kutembelea shamba la
malisho la mfugaji huyo lililopo Kijiji cha Msujile Kata ya Sejeli wilaya ya
Kongwa mkoani Dodoma ambapo aliridhishwa na ubora wa mifugo yake kutokana na
kupatiwa malisho bora. (17.07.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyevaa miwani) akikagua
malisho ya mifugo katika shamba la mifugo la Bw. Mnyonaki Saileni (aliyeshika
fimbo) alipofanya ziara katika shamba lake lililopo Kijiji cha Msujile Kata ya
Sejeli wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma ambapo aliitaka Taasisi ya Utafiti wa
Mifugo Tanzania (TALIRI) kuongeza wigo kwa wafugaji kuwa na mashamba ya
malisho. (17.07.2020)
DKT. NANDONDE ATEMBELEA KIWANDA CHA MOTHER DAIRIES LIMITED
Mkurugenzi wa uzalishaji na
Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Felix Nandonde jana alitembelea
kiwanda cha kusindika maziwa cha Mother Dairies Limited kilichopo Wilaya ya
Rufiji mkoani Pwani.
Katika ziara hiyo ya kikazi
Meneja wa uzalishaji wa kiwanda hicho Bw. Alle Makene alimweleza Dkt. Nandonde
kuwa kiwanda kina uwezo wa kusindika lita za maziwa 5000 kwa siku na sasa
kinasindika lita 2000 kwa siku sawa na asilimia 40 ya uwezo wa kiwanda hicho.
Kituo kinakusanya maziwa
kutoka kwa wafugaji kupitia vituo vitatu (Milk collection centres) ambapo
kiwanda kinanunua maziwa kwa bei ya shilingi 900 kwa lita moja kutoka kwa
wafugaji.
Kiwanda cha Mother Dairies
Limited kinatengeneza maziwa fresh na mtindi ambayo huuzwa katika masoko ya
mikoa ya Lindi, Dar es Salaam na Pwani.
Kiwanda hicho kina utaratibu
wa kuuza maziwa kabla ya kuwekwa kwenye vifungashio (bulk sale) kwa bei ya
shilingi 1200 kwa lita moja ya maziwa fresh na shilingi 1300 kwa maziwa ya mtindi.
Aidha, Bw. Makene alieleza
kuwa changamoto za tasnia ya maziwa ni pamoja na;
I. Upatikanaji wa maji baada
ya mfumo wa maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kuharibika tangu Mwezi
Machi, Mwaka 2020 na;
II. Ubovu wa miundombinu ya
barabara
Picha ya pamoja ya uongozi wa
kiwanda cha kusindika maziwa Mother Dairies Limited ukiwa na Kaimu Mkurugenzi
Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe, Bw. Gabriel Bura (wa
kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko Dkt. Felix Nandonde wote
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi mara baada ya kufanya ziara ya siku moja
katika kiwanda hicho kilichopo wilaya ya Rufiji mkoani Pwani baada ya kukagua
uzalishaji wa bidhaa ya maziwa. (16.07.2020)
Kipimo kinachotumika kukagua ubora
wa maziwa kabla ya kusindikwa katika kiwanda cha Mother Dairies Limited
kilichopo wilaya ya Rufuji mkoani Pwani. (16.07.2020)
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Felix Nandonde (wa kwanza kushoto)
akipata maelezo ya namna kiwanda cha kusindika maziwa cha Mother Dairies
kinavyofanya kazi kutoka kwa meneja uzalishaji wa kiwanda hicho, Bw. Alle
Makene. (16.07.2020)
Sehemu ya vifungashio vya
maziwa vinavyotumiwa na kiwanda cha kusindika maziwa cha Mother Dairies
kilichopo Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani. (16.07.2020)
ZIARA YA KATIBU MKUU UVUVI - FETA & TAFIRI
Mkandarasi kutoka kampuni ya
PETRA ENGINEERING, Eng. Basem Abu Ghalyoun akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu
Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (wa pili kutoka kulia
mbele) wakati wa ziara yake aliyoifanya ya kukagua maendeleo ya ujenzi kwenye taasisi
hiyo Dar es Salaam. (16.07.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto) akioneshwa michoro ya jengo
la Taasisi ya Utafiti wa masuala ya
Uvuvi (TAFIRI) wakati wa ziara yake aliyoifanya kwenye taasisi hiyo na Chuo cha
Uvuvi (FETA). (16.07.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (wa nne kutoka kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na
Menejiment ya chuo cha Uvuvi (FETA) wakati wa ziara yake chuoni hapo.
(16.07.2020)
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)