Mkurugenzi wa uzalishaji na
Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Felix Nandonde jana alitembelea
kiwanda cha kusindika maziwa cha Mother Dairies Limited kilichopo Wilaya ya
Rufiji mkoani Pwani.
Katika ziara hiyo ya kikazi
Meneja wa uzalishaji wa kiwanda hicho Bw. Alle Makene alimweleza Dkt. Nandonde
kuwa kiwanda kina uwezo wa kusindika lita za maziwa 5000 kwa siku na sasa
kinasindika lita 2000 kwa siku sawa na asilimia 40 ya uwezo wa kiwanda hicho.
Kituo kinakusanya maziwa
kutoka kwa wafugaji kupitia vituo vitatu (Milk collection centres) ambapo
kiwanda kinanunua maziwa kwa bei ya shilingi 900 kwa lita moja kutoka kwa
wafugaji.
Kiwanda cha Mother Dairies
Limited kinatengeneza maziwa fresh na mtindi ambayo huuzwa katika masoko ya
mikoa ya Lindi, Dar es Salaam na Pwani.
Kiwanda hicho kina utaratibu
wa kuuza maziwa kabla ya kuwekwa kwenye vifungashio (bulk sale) kwa bei ya
shilingi 1200 kwa lita moja ya maziwa fresh na shilingi 1300 kwa maziwa ya mtindi.
Aidha, Bw. Makene alieleza
kuwa changamoto za tasnia ya maziwa ni pamoja na;
I. Upatikanaji wa maji baada
ya mfumo wa maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kuharibika tangu Mwezi
Machi, Mwaka 2020 na;
II. Ubovu wa miundombinu ya
barabara
Picha ya pamoja ya uongozi wa
kiwanda cha kusindika maziwa Mother Dairies Limited ukiwa na Kaimu Mkurugenzi
Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe, Bw. Gabriel Bura (wa
kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko Dkt. Felix Nandonde wote
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi mara baada ya kufanya ziara ya siku moja
katika kiwanda hicho kilichopo wilaya ya Rufiji mkoani Pwani baada ya kukagua
uzalishaji wa bidhaa ya maziwa. (16.07.2020)
Kipimo kinachotumika kukagua ubora
wa maziwa kabla ya kusindikwa katika kiwanda cha Mother Dairies Limited
kilichopo wilaya ya Rufuji mkoani Pwani. (16.07.2020)
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Felix Nandonde (wa kwanza kushoto)
akipata maelezo ya namna kiwanda cha kusindika maziwa cha Mother Dairies
kinavyofanya kazi kutoka kwa meneja uzalishaji wa kiwanda hicho, Bw. Alle
Makene. (16.07.2020)
Sehemu ya vifungashio vya
maziwa vinavyotumiwa na kiwanda cha kusindika maziwa cha Mother Dairies
kilichopo Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani. (16.07.2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni