Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah hajaridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa
Jeongo la Utawala la Ofisi ya Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU)
unaoendelea katika Kisiwa cha Mafia.
Dkt. Tamatamah aliyasema hayo
baada ya kukagua kazi za ujenzi zinazoendelea ambapo hakuridhishwa na kasi ya
ujenzi kwani haiendani na muda uliotumika kwa mujibu wa mkataba.
"Sijaridhishwa na kasi
ya ujenzi niliyoikuta hapa hivyo ninakuagiza mkandarasi kuhakikisha unazingatia
ratiba na muda uliopangwa kulingana na mkataba" Alisisitiza Dkt.
Tamatamah.
Jengo hilo linasimamiwa na
mkandarasi mwelekezi "Y&P architects" linatarajiwa kutumiwa na MPRU
kama ofisi mara baada ya kukamilika kwake ambapo litasaidia kuongeza ufanisi wa
taasisi hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto), baadhi ya watendaji wa sekta
ya Uvuvi na baadhi ya watendaji wa kampuni ya "Y & P Architects" wakiangalia
hatua ya ujenzi iliyofikiwa kwenye jengo la Utawala la Ofisi ya Hifadhi ya Bahari
na Maeneo Tengefu (MPRU) lililopo kwenye kisiwa cha Mafia jana (18.07.2020).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni