Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw.
Gerald Kusaya leo (24.07.2020) ameongoza kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za
kisekta kujadili maandalizi ya Maonesho ya Kilimo Nane nane yatakayofanyika
kitaifa mkoani Simiyu kuanzia tarehe 01 Agosti, 2020.
Katika kikao hicho, Bw. Kusaya alieleza kuwa ni matarajio ya wizara ya kilimo
na zile za kisekta kuona maonesho ya Nane nane mwaka huu yanakuwa tofauti
katika kuleta mapinduzi ya, ufugaji na uvuvi ili wananchi wapate kuongeza tija
na ufanisi kukuza uchumi wa kaya na taifa.
Kikao hicho kimehusisha Makatibu
Wakuu ambao ni Prof. Riziki Shemdoe (Viwanda na Biashara), Prof. Elisante Ole
Gabriel (Mifugo), Mhandisi Anthony Sanga (Maji) na Dkt. Rashid Tamatamah
(Uvuvi) na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Miriam Mmbaga pamoja na kamati ya
maandalizi.
“Tunapenda kuona maonesho ya Nane
nane mwaka huu yanakuwa tofauti na yaliyopita katika kuwafanya wakulima, wafugaji
na wavuvi wabadilike kutoka katika kilimo cha kujikimu kuwa kilimo, ufaguji na
uvuvi wa kibiashara kupitia elimu na
teknolojia bora watakayojifunza kutoka kwa wataalam “ alisema Kusaya.
Kikao kimezishauri Wizara, taasisi na
wadau wa maonesho ya mwaka huu kujikita katika kuwasaidia wakulima,wavuvi na
wafugaji kuongeza tija katika shuguli zao ili baada ya maonesho maisha yao yawe
bora zaidi kiuchumi.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu (Mifugo)
Prof. Elisante Ole Gabriel alisema wakulima wanahitaji elimu ya kubadilisha
mtizamo hivyo matumizi ya vyombo vya habari kufikisha elimu kwa wakulima, wafugaji
na wavuvi ni muhimu sana kwenye maonesho haya.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara, Prof. Riziki Shemdoe alisema ni vema kamati ya uratibu ikaweka
utaratibu wa kuwakutanisha wafanyabiashara za mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi
pamoja na wakulima kwenye maonesho hayo hususan Simiyu.
“Tuandae maeneo kwa ajili wa
wafanyabiashara na wakulima, wafugaji na wavuvi kufanyia mazungumzo ya kukuza
upatikanaji wa masoko na kutumia fursa za biashara ikiwemo kuwekeza katika
viwanda” alisisitiza Prof. Shemdoe.
Maonesho ya Kilimo Nane nane mwaka
huu yana kauli mbiu isemayo “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua
Viongozi Bora 2020”.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ol Gabriel akizungumza
katika kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za kisekta kuhusu maandalizi ya
maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu. Kikao kimefanyika
katika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo. (24.07.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Kusaya
akiongoza kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara za kisekta kuhusu maandalizi ya
maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu. Kikao
kimefanyika katika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo. ( 24.07.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi),
Dkt. Rashid Tamatamah akizungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za
kisekta kuhusu maandalizi ya maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa
mkoani Simiyu. Kikao kimefanyika katika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa
Wizara ya Kilimo. (24.07.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.
Riziki Shemdoe akizungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za kisekta
kuhusu maandalizi ya maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani
Simiyu. Kikao kimefanyika katika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara
ya Kilimo. (24.07.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony
Sanga akizungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za kisekta kuhusu
maandalizi ya maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu.
Kikao kimefanyika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo. (24.07.2020)
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bibi Miriam Mmbaga
akizungumza kwenye kikao cha Makatibu Wakuu wa wizara za kisekta kuhusu
maandalizi ya ya maonesho ya Nane nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani
Simiyu. Kikao kimefanyika katika mji wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara
ya Kilimo (24.07.2020)
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia kikao cha
Makatibu Wakuu wa wa wizara za kisekta kuhusu maandalizi ya ya maonesho ya Nane
nane 2020 yatakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu. Kikao kimefanyika katika mji
wa serikali Mtumba katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo. ( 24.07.2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni