Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni
ya Ranchi ya Taifa (NARCO), Masele Mipawa amemsimamisha kazi Meneja wa Ranchi
ya West Kilimanjaro iliyopo Kilimanjaro, Hezron Kyaruzi kwa tuhuma za kukosa
uadilifu kwa mali za Umma na kusababisha upotevu wa Ng’ombe takriban 32.
Akiwa katika ziara ya
kutembelea Ranchi hiyo ya West Kilimanjaro Mipawa alisema kuwa waliamua kufanya
maamuzi hayo kufuatia changamoto nyingi zinazolikumba shamba hilo ambazo kwa
kiasi kikubwa zimechangiwa na uongozi mbovu wa meneja huyo.
“Kutokana na upotevu wa
Ngombe, uzembe na ukosefu wa maadili tumeamua kumsimamisha kazi Meneja wa
Ranchi na Msaidizi wake na hatua nyingine za kisheria na kinidhamu zitafuata ",
alisema Mipawa
Mipawa alisema ziara hiyo
aliyoifanya katika Ranchi hiyo ilikuwa na lengo la kufanya ukaguzi kutokana na
taarifa walizokuwa wakizipata ambazo zilionesha kuwa katika shamba hilo
kumetokea upotevu wa Ng’ombe ambao Kampuni ya NARCO haina taarifa nao.
Ziara hii pia imesaidia
kubaini kuwa kuna wizi uliokithiri katika shamba hili ambao umechangiwa na
mahusiano mabovu kati ya Meneja na jamii inayolizunguka shamba hilo, ukosefu wa
maadili na uadilifu wa Meneja ambao umepelekea
Ngombe 32 kupotea.
Kati ya ngombe hao 32
waliopotea 15 wameshapatikana na wengine 17 hawajapatikana mpaka sasa huku
ngombe wengine 27 walichinjwa bila kibali cha makao makuu, alifafanua Mipawa
Kufuatia hali hiyo, Mipawa
alisema wameamua pia kumsimamisha kazi Msaidizi wake kwa kuwa alishindwa
kumshauri vizuri meneja huyo huku ikidaiwa alikuwa akishirikiana na meneja huyo
kwenda kuazima ngombe kwa watu binafsi ili Ranchi hiyo ionekane ina idadi kubwa
ya ngombe.
Aidha, Mipawa aliwataka
wafanyakazi wengine waliobaki katika shamba hilo kuendelea kufanya kazi kwa
bidii, wazingatie nidhamu na uzalendo huku akiwaonya kuwa Serikali ya Awamu ya
Tano haitavumilia mtu yeyote anayehujumu rasilimali za Taifa.
Kaimu Meneja Mkuu - NARCO,
Bw. Masele Mipawa (aliyevaa suti nyeusi) akiongea na wafanyakazi wa Ranchi ya
West Kilimanjaro wakati alipokwenda kuangalia maendeleo ya ranchi hiyo.
(18.07.2020)
Kaimu Meneja Mkuu - NARCO,
Bw. Masele Mipawa akiwa amepanda farasi ambao wapo katika ranchi ya
West-Kilimanjaro wakati alipokwenda kukagua maendeleo ya ranchi hiyo.
(18.07.2020)
Kaimu Meneja Mkuu - NARCO,
Bw. Masele Mipawa akiongoza kikao cha watumishi wa Ranchi ya West-Kilimanjaro
wakati alipokwenda kukagua maendeleo ya ranchi hiyo. (18.07.2020)
Kaimu Meneja Mkuu - NARCO,
Bw. Masele Mipawa akiongoza kikao cha watumishi wa Ranchi ya West-Kilimanjaro
wakati alipokwenda kukagua maendeleo ya ranchi hiyo. (18.07.2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni