Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2020
Picha

HALMASHAURI ZASHAURIWA KUIGA MACHINJIO YA ILALA.

Picha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante Ole Gabriel amezishauri Halmashauri zote nchini ambazo zinafanya shughuli za ufugaji  kuiga mfano wa Machinjio ya kisasa ya Ilala ili nao waone haja ya kuwa na  machinjio ya kisasa yatakayosaidia kuboresha biashara ya machinjio na kuongeza pato la halmashauri zao. Profesa Ole Gabriel alitoa rai hiyo ofisini kwake jijini Dodoma Juni 26, 2020 alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Manispaa ya Ilala waliokuja kutembelea Machinjio ya Dodoma ili kujifunza namna ambavyo machinjio hayo yanavyoendeshwa. Akiongea na Wataalamu hao, Prof. Ole Gabriel alisema itapendeza kama kila halmashauri ikawa na machinjio ya kisasa kwani yatasaidia kuongeza mapato ya halmashauri hizo na kuachana na kukimbizana kila siku na waendeshaji wa machinjio yaliyopo sasa ambayo hayana viwango ambavyo vinatakiwa. “Niwaombe Makatibu Tawala wa Mikoa waliangalie hili, waone uwezekano wa kujenga machinjio ya kisasa yatakayosaidia kuboresha ...
Picha
WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI MHE. LUHAGA MPINA AFANYA UTENGUZI WA KAIMU MSAJILI WA BODI YA MAZIWA.

MADAKTARI WA MIFUGO WATAKIWA KUHUISHA TAARIFA ZAO.

Picha
Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania, Dkt.Bedan Masuruli amewataka Madaktari wa Mifugo nchini kuhuisha majina yao kwenye daftari la usajili wa madaktari wa mifugo  kabla ya  Julai 1, 2020. Wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma Juni 26, 2020, Dkt. Masuruli amesema ni muhimu wataalam kuhuisha majina yao ili baraza liweze kufahamu wako wapi, wanafanya nini na wanatoa huduma gani. "Nasisitiza madaktari wote wa mifugo ambao hawajahuisha taarifa zao kwenye daftari la usajili wa madaktari wafanye hivyo kuanzia leo hadi kufikia Juni 30, 2020 kwani kuanzia Julai mosi tunaanza kusimamia Sheria" amesema Dkt. Masuruli. Hata hivyo Dkt. Masuruli amesema wanafanya haya yote ili kuboresha huduma kwa wafugaji wote nchini na watatoa vitambulisho kwa wataalam wote ili wafugaji waweze kuwatambua.  Amesema kuwa wamejipanga kusambaza wataalamu wa mifugo kwenye ngazi za msingi ili kuwa karibu na wananchi na kuwashauri namna ya kuipatia kinga mifugo...

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI MHE. LUHAGA MPINA AFANYA UTEUZI.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amemteua Prof. Malongo Richard Mlozi kuwa Mwenyekiti  wa Bodi ya Wakala ya Vyuo vya Mifugo Tanzania(LITA) na amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya LITA. Kupata orodha ya wajumbe walioteuliwa  bofya hapa

MAGUFULI APONGEZA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli ameipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa jitihada kubwa ilizozichukua katika kipindi cha miaka mitano ya Uongozi wake ambazo zimesaidia kuboresha na kukuza uchumi wa nchi. Akizungumza wakati akitoa hotuba yake ya kulifunga Bunge la kumi na moja (11) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Juni 16, 2020 jijini Dodoma, Rais Magufuli alisema kuwa katika kipindi hiki cha miaka mitano ya uongozi wake Wizara ya mifugo imechukua hatua kadhaa ambazo zimesaidia nchi kufikia mafanikio makubwa. Rais Magufuli akitaja baadhi ya maeneo ambayo Wizara imeyashughulikia na kupata mafanikio, alisema kuwa katika kipindi hicho serikali iliongeza eneo la ufugaji kutoka hekta milioni 1.4 mwaka 2005 hadi kufikia hekta milioni 5 mwaka 2020. Jambo ambalo amelitaja kuwa limechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza migogoro kati ya Wakulima na Wafugaji. Kwa mujibu wa Rais Magufuli, Serikali kupitia Wizara imejenga mabwawa mapya ya kuogeshea n...

MHE. MPINA ATEUWA WAJUMBE WA BARAZA LA VETERINARI TANZANIA.

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (mb) kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 4(1) cha sheria ya veterinari Na.16 ya mwaka 2003 amewateuwa wajumbe wa Baraza la Veterinari Tanzania. kwa kuona majina ya wajumbe waliochaguliwa,  bofya hapa

UHUISHAJI WA MAJINA YA MADAKTARI KWENYE DAFTARI LA USAJILI.

Madaktari wafuatao wanatakiwa kuhuisha  majina yao kwenye daftari la usajili wa madaktari wa mifugo kabla ya tarehe 25/06/2020. kupata orodha ya madaktari ambao hawajahuisha majina yao,  bofya hapa

WADAU WA TASNIA YA NDEGE WAFUGWAO WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUTATUA KERO ZAO.

Picha
Wadau wa tasnia ndogo ya ndege wanaofugwa wameipongeza Serikali kwa kutatua kero za kisera ambazo zilikuwa zikidumaza tasnia hiyo.   Hayo yamesemwa na Katibu wa chama Kikuu cha Wadau wa Tasnia ya Kuku (PAT), Manase Mrindwa katika kikao cha Wadau wa tasnia ya kuku kilichofanyika jijini Dodoma Juni 18,2020. Akiongea kwenye kikao hicho Mrindwa alisema kuwa bajeti ya Serikali ya mwaka 2020/2021   imetoa majibu kwa kero zao kwa kuondoa kodi kwenye mayai ya kutotolesha vifaranga yanayotoka nje ya nchi, imepunguza tozo kwenye vyakula vya mifugo vinavyosafirishwa nje ya nchi na kupunguza  tozo kwenye mayai yanayosafirishwa nje ya nchi. “Unafuu huu wa tozo tunategemea utaiinua tasnia hii ya ndege wanaofugwa hapa Tanzania, alisema Mrindwa. Pamoja na pongezi hizo Mrindwa alieleza changamoto zilizowakumba kufuatia mlipuko wa maradhi ya Korona ambazo zimechangia kupungua kwa ulaji wa bidhaa za kuku kutokana na mdoror...

WATUMISHI WA SEKTA YA UVUVI WAASWA KUWA NA UADILIFU KATIKA UTUMISHI WA UMMA.

Picha
Watumishi wa sekta ya Uvuvi wameaswa kuwa na uadilifu katika utumishi wa Umma hasa katika kuzingatia sheria,Kanuni na Taratibu za Nchi. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah alipokua akifungua kikao cha Mafunzo ya maadili ya Utumishi wa Umma, yaliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper leo tarehe 18/06/2020. Dkt. Tamatamah amewasisitiza watumishi kuwa wazalendo katika kazi na kufuata maelekezo yote ya utumishi wa umma na sheria za Nchi. Lengo la mafunzo hayo ni kuwakumbusha watumishi kutambua majukumu yao ya kiutumishi pamoja na maadili ya utumishi wa umma. "Mtumishi anapaswa kujua misingi yake ya kazi katika utumishi na kuepuka kuchukua na kupokea rushwa katika kuwaudumia wananchi," alisema Dkt. Tamatamah. Naye Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma Bwana kutoka TAKUKURU, Joseph Kasongwa Mwaiselo amewaeleza watumishi madhara ya rushwa kwa serikali, na kwamba baadhi ya watumishi wamekuwa wakikumbatia rushwa na kudhani kuwa itawaongezea kipat...

BARAZA LA VETERINARI LAONYA MADAKTARI ‘FEKI’ KUHUDUMIA MIFUGO

Picha
Baraza la Veterinari nchini Tanzania limewataka watu wote ambao hawana sifa za Udaktari wa Mifugo kuacha mara moja kuhudumia na kutibu Mifugo huku likionya kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa watakao kwenda kinyume na Sheria. Onyo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Veterinari, Profesa Rudovick Kazwala katika Mkutano wa 45 wa Baraza hilo ulilofanyika jijini Dodoma Mei 4, 2020. Akiongea na Vyombo vya Habari mara baada ya Mkutano huo, Profesa Kazwala alisema kuwa kutokana na fani hiyo ya Udaktari wa Mifugo kuingiliwa na watu wasiokuwa na sifa Baraza limeamua kuandaa vitambulisho na beji vitakavyowatambulisha Madaktari hao pindi wanapokwenda kutoa huduma kwa wafugaji. “Wale wote wanaojiingiza katika fani hii bila kuwa na vyeti vya kitaaluma wajue kuwa kuna sheria namba 16 ya Veterinari ya mwaka 2003 ambayo inakataza mtu ambaye hajasomea taaluma ya Udaktari wa mifugo kufanya kazi ya kuhudumia na kutibu mifugo, atakayekutwa na kosa hilo sheria itachukua mkondo wake” a...

NAIBU WAZIRI ULEGA AAGIZA KUKAMILIKA KANUNI, KUSIMAMIA SHERIA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Abdallah Ulega, amewataka watendaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Uvuvi wa Bahari Kuu kufanya maandalizi ya kupata kanuni bora za kusimamia Sheria ya Uvuvi wa Bahari Kuu iliyopitishwa hivi karibuni na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akizungumza na watendaji wa mamlaka hiyo Mjini Unguja Visiwani Zanzibar akifuatana na Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili na Mifugo, Dkt. Makame Ali Ussi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ulega aliwataka watendaji hao kuunda kanuni bora zitakazoenda sambamba na mfumo wa biashara kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli anataka kuona namna ukanda wa bahari unavyosaidia kuinua uchumi wa taifa. “Jumla ya vipengele vyote vya sheria takriban 104 tumevifanyia kazi na vipengele kama 23 ambavyo havijaguswa lakini vingine vyote vimeguswa kuendana na uchumi wa bahari ili kuwa na mchango kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla katika kufanya m...