Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Mhe. Luhaga Mpina ameshiriki kwenye kikao cha kawaida cha mawaziri wa kilimo,
mifugo na uvuvi katika ukanda wa Afrika Mashariki ambacho kimetoka na maazimio
42.
Akizungumza mara baada ya
kutia sainia makubaliano hayo mawaziri wa nchi hizo, kwenye ukumbi wa mikutano
wa Afrika Mashariki (EACC) jijini Arusha Waziri Mpina ametaja maazimio manne
kati ya 42 ambayo yanalenga kubiresha sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.
Waziri Mpina amesema azimio
la kwanza ni nchi za Afrika Mashariki kuhakikisha zinazalisha chakula kwa kuongeza
uzalishaji na kuweka mikakati itakayowezesha kuwa na uzalishaji wa kutosha na
kujitosheleza kwa chakula.
Pili, kufanya biashara ya
mazao ya chakula mifugo na uvuvi kwa nchi za Afrika Mashariki kuwa na takwimu
za kujua kila nchi inafanya nini kwa kuwa na mfumo wa kupata takwimu kwa
kutumia mfumo wa aina moja.
Tatu, vijana
wanaoshughulika na kilimo, mifugo na uvuvi wengi wameshindwa kujiajiri na
kuajiriwa nchi za Afrika Mashariki zimetoka na azimimo la kuandaa mikakati ya
vijana kujiajiri na kuajiriwa katika sekta walizosomea za kilimo, mifugo na
uvuvi.
Aidha Waziri Mpina ametaja
azimimo lingine kuwa ni kutambua shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi ziende
sambamba na usimamizi wa matumizi ya kemikali hivyo kuzitumia kwa umakini ili
zisidhuru wananchi na mifugo.
Nchi zilizoshiriki kwenye
kikao hicho ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni