Wafugaji nchini mbioni
kunufaika baada ya wawekezaji kuja na nia ya kuwekeza kwenye mradi utakaohitaji
malighafi kutoka kwenye mifugo zikiwemo kwato,pembe,kinyesi na manyoya ambazo zitakuwa
zikinunuliwa kama malighafi nyingine ili kutumika kwenye kiwanda cha
kutengenezea mbolea.
Lengo la serikali ni
kuendelea kufungua milango kwa wawekezaji wote wenye nia ya kuwekeza kwenye maeneo
mbalimbali ikiwemo sekta ya mifugo nchini.Miradi kama hii itasaidia kuhamasisha
wananchi kuendelea kufuga kwa wingi na kwa tija baada ya kuona fursa za
uwekezaji zikiongezeka.
Hayo yamesemwa leo
(24/9/2019), na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Profesa Elisante
Ole Gabriel wakati akiwakaribisha wawekezaji wa kampuni ya ROKOSAN
inayojihusisha na utengenezaji wa mbolea kwa kutumia malighafi zitokanazo na mifugo
kutoka Jamhuri ya watu wa Slovakia kwenye makao makuu ya Wizara hiyo eneo la
mtumba jijini Dodoma.
Alisema wawekezaji walio
tayari kuwekeza wanakaribishwa na wizara inawaahidi ushirikiano wa hali ya juu
kwenye sekta ya mifugo kwa ajili ya kuinua hali za wafugaji wetu hapa nchini,
kuongeza ajira, pia kuongeza ukusanyaji wa kodi kupitia bidhaa mbalimbali
zikiwemo zile zitokazo viwandani.
Katibu Mkuu alisema
viongozi wa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzani Dkt.John Pombe Joseph Magufuli wanahitaji uwekezaji wenye matokeo ya
haraka na yenye tija kwa taifa ndio maana wizara yake iko tayari kutoa
ushirikiano pale mwekezaji anapoonyesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya mifugo
nchini.
Aidha Katibu Mkuu
aliwahakikishia kuwa Tanzania ni mahali salama na sahihi kwa uwekezaji huo kutokana
na rasilimali kubwa ya mifugo iliyopo nchini ambapo idadi ya ng,ombe ni
takribani milioni.32.2 mbuzi mil.20,kondoo 5.5, kuku mil.79.1 na punda zaidi ya
laki 6.
Prof.Gabiel aliongeza kuwa
uwekezaji huo nchini Tanzania utakuwa na manufaa sio kwa watanzania tu bali
hata kwa wawekezaji wenyewe kwa kuwa soko la bidhaa la ndani ya nchi ni kubwa,
Afrika ya Mashariki pia lipo,bila kusahau nchi wanachama wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Akizungumzia mradi huo wa
kiwanda cha kutengeneza mbolea kwa kutumia malighafi zitokanazo na mifugo
zikiwemo kwato, pembe, manyoya na kinyesi,Prof.Gabiel alisema itakuwa ni faraja
kwa wadau wa sekta kuona hakuna kinachotupwa kutoka kwenye mifugo bali
kinaongezewa thamani na kuwa bidhaa.
Profesa Gabriel aliongeza
kuwa hata kwenye Mpango Kabambe wa Kuendeleza Sekta ya Mifugo nchini (TLMP)
umeelekeza jinsi mnyororo wa kuongeza thamani malighafi zitokanazo na mifugo
zitakavyoleta tija kuelekea uchumi wa viwanda nchini.
Kwa upande.wake Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ROKOSAN Dkt. Stefan Szoke alisema anashukuru kwa
mwitikio wa serikali wa kuonyesha ushirikiano katika hatua za awali za
uwekezaji wa mradi huo.
Dkt. Szoke alisema baada ya
kufuatilia masuala ya uwekezaji waligundua kuwa Tanzania ni nchi yenye fursa
kubwa za uwekezaji kutokana na rasilimali na mazingira mazuri yaliyopo katika
sekta ya mifugo na kusisitiza kuwa nia yao ni kuanzisha miradi yenye manufaa
kwa haraka mara baada ya kukamilisha taratibu husika.
Akitolea mfano nchi za
Ulaya ambako pia wamewekeza miradi ya aina hiyo, Dkt.Szoke alisema licha ya wafugaji
kunufaika kwa kuuza malighafi hizo zitokanazo na mifugo, wakulima nao wamekuwa wakinufaika
kwa kupata mbolea yenye ubora na kwa gharama nafuu.
Akifafanua faida nyingine
ya mradi huo alisema kuwa gharama za uzalishaji zikipungua hata bei ya mazao
sokoni hupungua hivyo kumfanya mwananchi kumudu bei za bidhaa mbalimbali ziwemo
za vyakula ambayo ni muhimu kwa afya zao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni