ZIARA YA KATIBU MKUU UVUVI
DKT. RASHID TAMATAMAH MKOANI RUKWA.
Dkt. Rashid Tamatamah amesema
mikakati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi hasa kwenye Sekta ya Uvuvi ni kuendeleza
ufugaji samaki na kuangalia fursa za kuwekeza katika ufugaji samaki.
Hayo yamebainishwa na katibu
Mkuu Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah alipofanya ziara
yake leo (15/07/2019) Mkoani rukwa ya kutembelea bwawa la Ilembo, Kiwanda cha kuchakata
samaki cha Migebuka Fisheries, soko la Kasanga Pamoja na kuwatembelea Watumishi
wa kituo cha Doria cha Kasanga.
▶FURSA
ZA UWEKEZAJI KATIKA UFUGAJI SAMAKI.
Serikali ipo hapa na nia yetu
ni kuja na kusikiliza changamoto zinazowakabili katika suala zima la ufugaji samaki.
Serikali ipo hapa na nia yetu
ni kuangalia fursa ya kukuza Tasnia ya ukuzaji viumbe maji hasa ufugaji wa samaki
na kuwekeza katika malambo ambapo yakitunzwa vizuri yanaweza kutoa samaki wengi
kwa wananchi.
Katibu Mkuu Uvuvi Dkt. Rashid
Tamatamah amesema hayo leo alipopata fursa ya kutembelea bwawa la Ilembo na
kuongea na Wananchi wa Kijiji cha Ilembo, Katika Wilaya ya Sumbawanga.
Lengo la ziara hii ni kuja
kuangalia fursa ya maeneo ya kupandikiza samaki kwenye mabwawa,alisema Katibu
Mkuu Uvuvi.
Malambo yanayoweka maji mwaka
mzima tunataka kuyapandikiza samaki ili wananchi waendelee kupata samaki.
Vilevile kuangalia namna
Wizara itakavyotoa mchango kwa Watanzania wanaopata changamoto ya kuingia
katika ufugaji samaki.
Pia Dkt. Tamatamah alieleza
kuwa, watu wahamasike kufuga samaki kwenye mabwawa na wasitegemee maziwa peke
yake ili kujiongezea kipato.
▶UDHIBITI
WA UTOROSHAJI SAMAKI, KULINDA VIWANDA VYA NDANI.
Katibu Mkuu Dkt. Rashid
Tamatamah amesema nia ya Mh. Raisi Dkt. John Pombe Magufuli haitafikia ya Serikali
ya viwanda kama malighafi yote inakimbizwa nchi za nje.
Alisema hayo leo wakati
alipotembelea Kiwanda cha kuchakata samaki cha Migebuka Fisheries kilichopo
Kasanga, Wilaya ya Kalambo.
Afisa Mfawidhi kituo cha
Rukwa na Katavi Bw. Juma Makongororo amesema, Nguvu kazi ikiongezeka itasaidia kudhibiti
uingizaji holela wa mazao ya Uvuvi na dhana haramu za uvuvi.
▶UIMARISHAJI
WA SOKO LA KASANGA
Sisi kama Wizara ya Mifugo na
Uvuvi, kipaumbele chetu ni kuimarisha miundo mbinu ya masoko ya samaki.
Alisema hayo Katibu Mkuu
Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah alipotembelea Soko la samaki la Kasanga, Wilaya ya
Kalambo Leo na kuongea na uongozi wa eneo hilo la soko.
Kwa niaba ya Wizara napenda
kuchukua nafasi hii kushukuru Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kwa juhudi ya
kuendelea kuimarisha soko la Kasanga alisema
Katibu Mkuu.
Mara nyingi kuimarisha masoko
ya ndani yanaongeza thamani ya samaki na kupata soko la nje na kusaidia kukuza
uchumi wa nchi.
▶KIKAO
KAZI KITUO CHA DORIA KASANGA
Katibu Mkuu Dkt. Rashid
Tamatamah alipata wasaa wa kuongea na Watumishi wa kituo cha Doria cha Kasanga
na kusikiliza changamoto za kazi zinazowakabili katika maeneo yao.
katibu Mkuu Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashid
Tamatamah afanya ziara yake leo (15/07/2019) Mkoani rukwa ya kutembelea kiwanda
cha kuchakata Samaki cha Migebuka Fisheries kilichopo Kasanga
katibu Mkuu Uvuvi,
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah leo (15/07/2019) akutana na
kuongea na Watumishi wa Kituo cha Doria cha Kasanga, Mkoani Rukwa
katibu Mkuu Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah
afanya ziara yake leo (15/07/2019) Mkoani rukwa ya kutembelea bwawa la Ilembo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni