Katibu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid
Tamatamah amewataka washiriki wa mafunzo ya siku sita ya uelewa wa ufuatiliaji wa ubora na unadhifu wa
maji na mazingira kuzingatia mafunzo hayo ili yawe na tija katika ukanda wa Bahari ya Hindi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam (30.06.2019) wakati wa
kufunga mafunzo hayo yaliyokuwa yakifanyika katika Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) Dkt.
Tamatamah amesema mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Serikali ya Watu wa China kupitia
Sino-Africa Joint Research Centre (SAJOREC) na East African Great Lakes Urban Ecology (EAGLU) kwa kushirikiana
na TAFIRI yanalenga kuboresha sekta ya uvuvi nchini pamoja na nchi zinazonufaika na Bahari ya Hindi
pamoja na maziwa yaliyopo nchini.
Kuhusu mafunzo hayo katibu mkuu huyo Dkt. Tamatamah amesema
washiriki walipata mafunzo kupitia mihadhara iliyotolewa na wakufunzi wabobezi kutoka China na
Tanzania pamoja na kukusanya takwimu kutoka mito iliyopo Mkoani Dar es Salaam na kuchakata
takwimu hizo katika maabara ya TAFIRI.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAFIRI Dkt. Semvua
Mzighani amesema kupitia mafunzo hayo Serikali ya Watu wa China, SAJOREC na EAGLU wametoa
vifaa vya utafiti vyenye thamani ya Tshs Milioni 70 ambavyo vitatumika kwa tafiti za kuangalia ubora
na unadhifu wa maji na mazingira kwa ujumla.
Aidha Dkt. Mzighani amesema mafunzo hayo yalishirikisha
washiriki kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Ethiopia pia walikuwepo waendesha
mafunzo hayo kutoka China.
Vifaa vyenye thamani ya Tshs Milioni 70 vilivyotolewa katika
Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) na Serikali ya Watu wa China kwa
kushirikiana na Sino-Africa Joint Research Cente (SAJOREC) na East African
Great Lakes Urban Ecology (EAGLU) wakati wa mafunzo ya ufuatiliaji ubora na
unadhifu wa maji pamoja na mazingira yaliyofanyika TAFIRI kwa siku sita.
|
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah wakati akifunga mafunzo ya siku
sita ya ufuatiliaji ubora na unadhifu wa maji pamoja na mazingira yaliyofanyika
katika Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) ambapo pia aliwakabidhi pia
washiriki vyeti vya ushiriki wa mafunzo hayo.
|
x
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni