Serikali kupitia
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeteketeza Tani 11 za samaki zenye thamani ya zaidi
ya Tshs mil.60 zilizobainika kuwa na sumu na hazifai kwa matumizi ya binadamu.
Tukio hilo la
uteketezaji wa samaki wenye sumu limefanyika leo likiongozwa na Waziri wa
Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Joelson Mpina (Mb) katika eneo la dampo
lililopo Pugu Kinyamwezi Jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo imefikiwa
na serikali baada ya Mahakama kuridhia kuwa samaki hao walioingizwa nchini si
salama kwa matumizi ya binadamu.
“Lengo ni
kuhakikisha rasilimali za uvuvi zinakuwa endelevu, zinavuliwa salama ili
ziendelee kuwepo katika kizazi cha sasa na kizazi kijacho, ”alisema Mh.Mpina.
Pia Waziri Mpina
alisema, Watanzania wako Salama hakuna namna yoyote mazao ya uvuvi yanaweza
kuwafikia yakiwa hayajapimwa na kuthibitishwa.
Aidha Mhe. Mpina
amezitaka Taasisi za Serikali zinazohusika na udhibiti na usimamizi wa sekta ya
uvuvi kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana ili kuhakikisha watanzania
wanatendewa haki katika biashara za ndani na nje ya nchi.
“Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe
Magufuli inahakikisha ipo kwa ajili ya kumlinda Mtanzania asiweze kupata
madhara yoyote na kuwa salama”. alisema Mpina.
SERIKALI YATEKETEZA TANI 11 ZA SAMAKI ZENYE THAMANI YA Sh.MIL 66 |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni