AMEPOTEA
NICKSON .K. KEIYA
AMBAYE NI MTUMISHI WA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KAMA MENEJA WA
SHAMBA LA KUZALISHA MITAMBA LA SAO HILL L.M.U LILILOPO WILAYANI MAFINGA MKOA WA
IRINGA AMEPOTEA TANGU 15/01/2019 AKIWA NA PIKIPIKI YENYE NAMBA YA USAJILI MC
214 BZZ AINA YA KING LION NYEKUNDU KATIKA MAENEO YA ILUNDI/MISITU YA SAO HILL.
TAARIFA ZA KUPOTEA KWAKE ZIMERIPOTIWA KITUO CHA POLISI MAFINGA –
IRINGA.
KWA MARA YA MWISHO ALIKUWA AMEVAA SURUALI YA KAKI NA SHATI LENYE
RANGI YA UDONGO YENYE MICHIRIZI MYEUPE NA RABA ZA RANGI YA KAKI YENYE SOLI
NYEUPE.
KWA ATAKAYEMUONA TUNAOMBA ATOE TAARIFA KWENYE KITUO CHOCHOTE CHA
POLISI KILICHOPO KARIBU NAE.
AU APIGE SIMU NAMBA
• 0713 757157
• 0762 952766
Imetolewa na R. Mbulalina.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
DODOMA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni