MAJIBU YA SERIKALI KUHUSU HOJA ZILIZOIBULIWA NA WAVUVI KUPITIA GAZETI LA NIPASHE LILILOKUWA NA KICHWA CHA HABARI ‘WAVUVI WATAKA BEI ELEKEZI SANGARA’ LA TAREHE 22 NOVEMBA, 2018 NA. HOJA MAJIBU 1. Kukosekana kwa bei elekezi ya Sangara Kufuatia malalamiko ya wavuvi kuhusu bei ya Sangara, Mhe Waziri wa Mifugo na Uvuvi alishafanyia kazi suala hilo ambapo akiwa Kanda ya Ziwa, alifanya mkutano na wamiliki wa viwanda na bei elekezi ilitolewa kwamba kwa kila kilo moja ya Sangara bei itakuwa ni Tsh. 5,500/= . Aidha, wadau wa viwanda pia walikiri kwa barua kwamba watatekeleza bei elekezi kama ilivyoamriwa. 2. Kukandamizwa na kunyanyaswa kwa wavuvi na wanaosimamia sheria Operesheni zinazoendelea zinatekelezwa kwa mujibu wa Sheria za Nchi zikiwemo:- Sheria ya Uvuvi Namba 22 ya Mwaka 2003 pamoja na Kanuni zake za Mwaka 2009; Sheria ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya Mwaka 1998 na marekebish...
Machapisho
Inaonyesha machapisho kuanzia 2018
KIKAO KAZI CHA WAZIRI MH. LUHAGA MPINA NA WASINDIKAJI WAKUBWA WA MAZIWA NCHINI.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Joelson Mpina (Mb) amekutana na Kampuni kubwa za usindikaji wa maziwa nchini (Tanga Fresh, ASAS,MILCOM NA AZAM) leo tarehe 12/11/2018 jijini Dodoma. Lengo la kikao kazi hicho ilikuwa ni kujadili mikakati ya uongezaji wa Usindikaji wa maziwa kwenye Kampuni kubwa za Maziwa nchini. Nataka Ifikapo tarehe 12/12/2018 mkakati wa ushirikiano uwe umekamilika na kusainiwa kati ya Kampuni za Wasindikaji wa Maziwa na Dawati la Sekta Binafsi, alisema Mh.Waziri Luhaga Mpina. Mhe. Mpina aliwaelekeza Wakuu wa Idara na Vitengo kila mtu kwa upande wake kulitumia na kulisimamia dawati katika kutekeleza Mikakati iliyopangwa. Mkakati huu unaenda kuongeza uzalishaji wa maziwa kwa asilimia 84.7 kwa mwaka, alisema Mpina. Tunazindua mkakati wa dawati tarehe 15/12/2018 na kwenda kuwakabidhi mitamba 350 kwa wafugaji wa Chama Kikuu-Tanga kama shukurani kwa jitihada za wenzetu wa TADB, Mpina. Serikali imefanya jitihada kubwa k...
MAKATIBU WAKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI WASISITIZA USHIRIKIANO KATI YA WATUMISHI WA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Kufuatia kikao cha watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kilichofanyika Leo tar 7/11/2018 katika ukumbi wa VETA DODOMA Katibu Mkuu Mifugo ahamasisha yafuatayo:- Ushirikiano kati ya watumishi ni jambo la Msingi sana ili kuweza Kufanikisha shughuli zetu za kila siku pia ni lazima tufanye kazi kwa kujituma. Changamoto siyo sehemu ya maisha ila changamoto ndiyo maisha yenyewe, kwa hiyo tunazitumia hizo changamoto kama fursa. Wakurugenzi na wakuu wa vitengo jitahidini sana kuwasikiliza mnaowaongoza ,na kuwasimamia na kubwa zaidi kujali maslahi yao. Nataka Wizara hii iende kwa kasi sana ,Idara ya Uzalishaji na Masoko Ikiwa kama Operating Engine kwa sababu ndiyo yenye activities nyingi sana Pia napenda kuwataarifu rasmi kuwa Dr. Angelo Mwilawa kuanzia sasa nimemteua kuwa Mkurugenzi Rasmi wa Idara ya Ugani na mafunzo (DRTE) hapo awali alikuwa anakaimu. KMU asisitiza Sekta...
PROJECT LAUNCHING WORKSHOP, 07 NOVEMBER,2018. AT MORENA HOTEL DODOMA.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
NEW ZEALAND KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), amekutana na Balozi wa New Zealand Nchini Tanzania Mike Burrell Ofisini kwake leo tarehe 06/11/2018 jijini Dodoma. Tumekuwa tukishirikiana vyema kati ya Nchi ya Tanzania na New Zealand katika kupata madume bora ya Ng’ombe 6 kule kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC) kilichopo UsaRiver jijini Arusha ambayo yamechangia uzalishaji wa mbegu bora kuongezeka zaidi, alisema Mh. Ulega. Mh.Ulega alisema tutasaidiana katika upande wa ufugaji wa samaki, ambapo wenzetu wako mbele zaidi katika masuala ya Ukuzaji viumbe kwenye maji. “ Our President Dkt. John P. Magufuli is trying so hard to ensure that, our environment in Tanzania is getting better and better”. Say’s Ulega. Vilevile Mhe. Ulega alisema kunahitajika watu wa kwenda kusoma katika kada ya Sayansi ambapo kwa sasa bado tunapeleka watu wachache katika fani hiyo. Kwa upande wake balozi Mike alisema, tunahitaji Ushirikiano na Tanzana katika kuwekeza ...
WAKURUGENZI WAPYA WATAMBULISHWA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Katibu Mkuu Mifugo Prof. Elisante Ole. Gabriel leo atambulisha Wakurugenzi wapya katika kikao cha Wakuu wa Vitengo na Idara kilichofanyika katika Ukumbi wa NBC Leo. # Prof. O. Gabriel, alisisitiza Wakurugenzi kujifunza kwa watu na kuwa na Ushirikiano. #KM aliwataka Wakurugenzi kuwa wabunifu katika kazi zao ili kuinua Sekta. # Prof. aliwaomba Wakurugenzi kukabiliana na changamoto zilizopo na kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kuzitatua. # Alisisitiza kujenga utamaduni wa Kushirikiana kwa pamoja na kufanya kazi kwa Ushirikiano. Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel ampongeza na kumkaribisha Kaimu Mkuu mpya wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi. Rehema ,bulalina, leo katika ukumbi wa NBC KM Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel ampongeza na kumkaribisha Mkurugenzi mpya wa Idara ya Huduma za Mifugo Dkt. H. Nonga, Leo katika ukumbi wa NBC KM Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel ampongeza na kumkaribisha Mkurugenzi mpya wa I...
KATIBU MKUU ATEMBELEA SOKO LA SAMAKI FERRY KUKAGUA UJENZI WA VYOO:
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Leo Katibu Mkuu wa Uvuvi Dkt. Rashid Tamatama alikwenda kuangalia utekelezaji wa ujenzi wa vyoo 24 hiyo ikiwa ni katika hatua za utekelezaji wa ahadi za Mh. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina alipotembelea sokoni hapo na kubaini mapungu yaliyopo ikiwemo. 1. Uchakavu wa majengo 2. Upungufu wa vyoo; 3. Kujaa kwa mchanga katika bahari: na 4. Uchakavuwa jokofu la kuhifadhia samaki Ambapo alisema kuwa Wizara yake itaingilia kwa kuchukua hatua za haraka katika hayo na kuagiza mara moja kwa ujenzi wa vyoo 24 ambavyo vitapunguza msongamano sokoni hapo. Katibu Mkuu wa Uvuvi, Dkt. Rashidi Tamatamah ametembelea soko la samaki Ferri- Kivukoni kuangalia ujenzi wa vyoo 24 ambavyo vitapunguza msongamano katika soko hilo. Katibu Mkuu Uvuvi, akielekea eneo la ujenzi akiambatana na Meneja wa soko Bw. Mkuu Anje Katibu Mkuu Uvuvi akiwa katika eneo la Ferry Katibu Mkuu akiwa na Meneja wa soko hilo akifafanua jambo sokoni hapo Choo ambacho ki...
SERIKALI IPIME MAENEO YA WAFUGAJI ILI WAMILIKISHWE KISHERIA
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Wafugaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro wamewalalamikia watendaji wa Serikali na kwamba wao ndio wanao chochea Migogoro kati ya Wakulima na Wafugaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai. Malalamiko hayo yametolewa jana na wafugaji wa kijiji cha Sanya Station, katika kata ya Kia, katika Halmashauri ya Wilaya Hai, walipokuwa wakitoa kero zao kwa Katibu Mkuu Mifugo, Prof.Elisante Ole Gabriel, aliyefika katika kijiji hicho kusikiliza kero za wafugaji hao kwa Niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe .Luhaga Joelson Mpina. “Sisi Wafugaji na Wakulima natuna tatizo kabisa, Shida kubwa iko kwa hao Mgambo, ambao wanatumwa na watendaji wa Serikali waje wakamate Ngombe wetu bila kosa lolote na kufanya mradi wao wa kuwaingizia fedha;.alisikika Mfugaji akilalamika. Aidha watumishi waliopo katika taasisi za Umma za NARCO na TALIRI ,West Kilimanjaro nao wamelalamikiwa na wafugaji hao kuwa ni vinara wa kuchukua rushwa hasa Ngombe wa wafugaji wan...
SERIKALI YATEKETEZA NYAVU ZA WAVUVI HARAMU NYUMBA YA MUNGU
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Serikali imepiga marufuku uvuvi haramu na kuteketeza nyavu aina ya makokoro 35 , makila 6 na nyavu za zenia 25 zilizokuwa zikitumiwa na wavuvi haramu katika bwawa la Nyumba ya Mungu lililopo Mkoani Kilimanjaro Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kagongo kata Lang’ata leo amesema serikali haitamwonea huruma mtu yeyote atakayekamatwa akijihusisha na uvuvi haramu kwani serikali imekua ikipoteza kiasi kikubwa cha mapato kutokana na uvuvi huo. “Hatuna utani na mtu asiye na huruma na rasilimali za nchi hii, Tanzania ndio nchi yenye sehemu kubwa yenye maji kuliko sehemu nyingine lakini bado tunaagiza samaki kutoka nchini china, tumeagiza sato., perege hadi kibua wa kichina, tusipotokomeza leo bwawa litakuwa historia kwa vizazi vijavyo” amesema Ulega Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alisema uwepo wa bwawa hilo umekuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika eneo hilo na sasa ni wakati wa wananchi kuwa walin...
UZINDUZI WA BODI YA KAMPUNI YA RANCHI ZA TAIFA (NARCO)*
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Bodi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) imezinduliwa rasmi tarehe 27/10/2018 na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Joelson Mpina. Ninawashukuru wote kwa kukubali uteuzi huu kwa sababu natambua hakuna kazi iliyo nyepesi - Waziri Mpina Namshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa uteuzi huu kwani ametambua uwezo na uzalendo wenu, Nchi hii inapaswa kuendelezwa na wananchi wazalendo watakaowezesha Nchi kusonga mbele - Mhe. Mpina Ni matarajio yangu kuwa; Bodi hii itaweza kufikia Mikakati tuliojiwekea na ndani ya Wiki mbili zijazo lazima kikao cha Bodi kiitishwe ili kuanza utekelezaji wa mikakati tutakayojiwekea - Waziri Mpina Sekta ya Mifugo ina mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa letu ambapo mpaka sasa jumla ya Mifugo tuliyonayo ni mil 57 na tunazalisha Lita Bil 2.4 za Maziwa - Waziri Mpina. Tunahitaji mpaka mwakani tuongeze idadi kubwa ya Mifugo kwa sasa, tuna Ngombe milioni 30.5, mbuzi 18.8 mil, kondoo Mil. 5.3, nguruwe Mil. 1.9, Kuku wa kienyeji Mil. 38.2, na wa kisasa ni ...
KATIBU MKUU MIFUGO, PROFESA ELISANTE OLE GABRIEL AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA OMAN MHE. ALI A. AL MAHRUQI NCHINI TANZANIA JUU YA KUTAFUTA SOKO LA NYAMA NCHINI OMAN.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Katibu Mkuu ( mwenye suti nyeusi ) na Balozi wa Oman wakiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa kutoka Wizara ya mambo ya nje na wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel akisema jambo kwenye kikao kifupi mapema leo jijini Dar es salaam. Katibu Mkuu Profesa Elisante Ole Gabriel akijadili jambo na Balozi wa Oman Mhe. Ali A. Al Mahruqi mapema leo jijini Dar es salaam.
KATIBU MKUU MIFUGO AFANYA UKAGUZI MINADA YA SHANWA MASWA NA MWANUZI MEATU
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof.Elisante Ole Gabriel leo amefanya ukaguzi mnada ya Awali wa Shanwa uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa na Mwanuzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu. Akiongea na Katibu Mkuu, Dkt. Gabriel Bura kutoka Wizarani ambaye pia ni mmoja wa timu Nzagamba, Dkt. Bura,amemweleza Katibu Mkuu kuwa tangu wamewasili hapo, kazi zinaenda vizuri bila shida yoyote. Katibu Mkuu tangu timu Nzagamba imeanza kutekeleza majumu yake,katika mnada wa Senai timu ilifanikiwa kukusanya jumla ya Tsh.7,028,000/= ukilinganisha na Tsh.756,000/= zilizokuwa zinakusanywa kabla ya Nzagamba kuanza kutekeleza Majukumu yake. alisema. Aidha Bura amesema kuwa wafanyabiashara wameanza kuelewa mabadiliko ya tozo mpya,isipokuwa bado kuna changamoto chache, baadhi ya wafanyabiashara wanafanya biashara nje Minada kinyume cha sheria ili kukwepa kwa Makusudi kulipa tozo zilizowekwe kisheria. Wakati huo huo baadhi ya wafugaji waliokuwepo katika mnada w...
ULEGA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA NNE YA NDEGE WAFUGWAO
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega amezindua rasmi maonesho ya nne ya ndege wafugwao katika viwanja vya maonesho (sabasaba) jijini Dar es salaam. Akizungumza katika uzinduzi huo Ulega ameeleza kuwa maonesho ya mwaka huu yamehusisha makampuni mengi ya ndani na nje ya nchi kama Kenya, Poland na China na amewakaribisha kuwekeza nchini kutokana na kuwepo kwa fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali. Aidha ametoa pongezi kwa vyama vyote vya wadau wa ndege wafugwao chini ya chama mama cha Tanzania Poultry show (TPS) kwa kutoa kipaumbele katika suala la ufugaji wa kuku. Pia amewataka kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na wao kama serikali wapo pamoja kama walezi wao, katika kuhakikisha wanasonga mbele zaidi na amewapongeza kwa ushirikiano wao kupitia vyama vyao. Ulega amesema kuwa Rais Magufuli ameendelea kusimamia maendeleo ambapo hadi sasa tozo zilizokuwa kero kwa wafugaji, wakulima na wavuvi zimeondolewa ili kuweza ...