Serikali imepiga marufuku uvuvi haramu na kuteketeza nyavu
aina ya makokoro 35 , makila 6 na nyavu za zenia 25 zilizokuwa zikitumiwa na wavuvi haramu katika
bwawa la Nyumba ya Mungu lililopo Mkoani Kilimanjaro
Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega akizungumza na
wananchi wa kijiji cha Kagongo kata Lang’ata leo amesema serikali haitamwonea huruma mtu yeyote
atakayekamatwa akijihusisha na uvuvi haramu kwani serikali imekua ikipoteza kiasi kikubwa cha
mapato kutokana na uvuvi huo.
“Hatuna utani na mtu asiye na huruma na rasilimali za nchi
hii, Tanzania ndio nchi yenye sehemu kubwa yenye maji kuliko sehemu nyingine lakini bado tunaagiza
samaki kutoka nchini china, tumeagiza sato., perege hadi kibua wa kichina, tusipotokomeza leo bwawa
litakuwa historia kwa vizazi vijavyo” amesema Ulega
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira
alisema uwepo wa bwawa hilo
umekuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika eneo hilo na sasa
ni wakati wa wananchi kuwa walinzi kwa kila mmoja ili kutokomeza uvuvi haramu.
“Hebu leo amueni kabisa kwamba biashara ya samaki ndio mfumo
wa maisha yenu, Ninyi mkifanya
hivyo sisi hatutahitaji kufunga hili bwawa , wakati wote
tutahitaji kuongeza kizazi cha samaki na kuleta wataalamu kupima kiwango cha samaki tulichonacho” alisema
Mghwira
Kwa upande wake Dismas Gondwe mkazi wa kijiji cha kigongo
kata ya Lang’ata amesema uvuvi haramu katika bwawa hilo unatokana na kukosekana kwa utaratibu
maalumu unaowaelekeza wavuvi kuendesha shughuli zao katika bwawa hilo.
Gondwe ameiomba serikali kuwawezesha wavuvi wa bwawa la
Nyumba ya Mungu zana harali ambazo serikali inazitambua.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega (wa kwanza kulia) kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro , Anna Mghwira na Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Aatron Mbogho wakiteketeza zana haramu zilizokuwa zikitumika katika uvuvi haramu kwenye Bwawa la Nyumba ya Mungu. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni