Kufuatia kikao cha watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,
kilichofanyika Leo tar 7/11/2018 katika ukumbi wa VETA DODOMA Katibu Mkuu Mifugo ahamasisha
yafuatayo:-
Ushirikiano kati ya watumishi ni jambo la Msingi sana ili
kuweza Kufanikisha shughuli zetu za kila siku pia ni lazima tufanye kazi kwa kujituma.
Wakurugenzi na wakuu wa
vitengo jitahidini sana kuwasikiliza
mnaowaongoza ,na kuwasimamia na kubwa zaidi kujali
maslahi yao.
Nataka Wizara hii iende kwa kasi sana ,Idara ya Uzalishaji na
Masoko Ikiwa kama Operating Engine kwa sababu ndiyo yenye activities nyingi sana
Pia napenda kuwataarifu rasmi kuwa Dr. Angelo Mwilawa kuanzia sasa nimemteua kuwa Mkurugenzi Rasmi wa Idara ya
Ugani na mafunzo (DRTE) hapo awali alikuwa anakaimu.
KMU asisitiza Sekta zote mbili kuwa na ushirikiano |
KMM akiongea na watumishi ( hawapo pichani) na kusisitiza ushirikiano katika kazi |
KMM na KMU wakiteta jambo na Mkurugenzi msaidizi wa Ukuzaji Viumbe kwenye maji |
Picha ya pamoja Makatibu Wakuu, Wakurugenzi na Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi |
Makatibu Wakuu, wakiwa naWakuu wa Idara, Vitengo na Tahasisi katika picha ya pamoja |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni