Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga
Abdallah Ulega amezindua rasmi maonesho ya nne ya ndege wafugwao katika viwanja
vya maonesho (sabasaba) jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika uzinduzi huo Ulega ameeleza kuwa maonesho
ya mwaka huu yamehusisha makampuni mengi ya ndani na nje ya nchi kama Kenya,
Poland na China na amewakaribisha kuwekeza nchini kutokana na kuwepo kwa fursa
za uwekezaji katika sekta mbalimbali.
Aidha ametoa pongezi kwa vyama vyote vya wadau wa ndege wafugwao
chini ya chama mama cha Tanzania Poultry show (TPS) kwa kutoa kipaumbele katika
suala la ufugaji wa kuku.
Pia amewataka kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na
wao kama serikali wapo pamoja kama walezi wao, katika kuhakikisha wanasonga
mbele zaidi na amewapongeza kwa ushirikiano wao kupitia vyama vyao.
Ulega amesema kuwa Rais Magufuli ameendelea kusimamia maendeleo
ambapo hadi sasa tozo zilizokuwa kero kwa wafugaji, wakulima na wavuvi
zimeondolewa ili kuweza kuendeleza shughuli hizo.
Kuhusiana na
changamoto zilizotolewa na wafugaji hao hasa katika mashudu na soya ambazo huagizwa
kutoka nje Ulega amesema kuwa maandalizi yameanza katika nyanda za juu kusini
ambako soya zimelimwa na wanavutia uwekezaji katika usindikaji ili kuweza
kuvutia uwekezaji wa kuchakata soya na kupunguza gharama za kuagiza bidhaa hizo
kutoka nje.
Kuhusiana na machinjio zinazochinja kuku Ulega amesema kuwa sehemu
hizo zimekuwa na ubora wa chini sana na amewataka wahakikishe wanaboresha
machinjio hayo yanayosimamiwa na halmashauri na manispaa hasa kwa kuzingatia
wanaweka sehemu ya machinjio ya kuku ili kuleta thamani.
Mwenyekiti wa chama cha ndege wafugwao Harko Bhaghat amemshukuru
Naibu Waziri na Wizara kwa ujumla kwa kutoa kipaumbele kwa wafugaji na kusema
kuwa hadi sasa wamepata mafanikio makubwa na kubwa zaidi ni baada ya serikali
kuondoa tozo katika bidhaa za mifugo.
Bhaghati amewataka wafugaji kujisajili ili waweze kupata
fursa mbalimbali za kuendeleza soko la ndege wafugwao hasa kuku.
Mtaalamu na Mshauri wa Mifugo kutoka kampuni ya Hill Poultry Feed akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega kuhusu uzalishaji na utunzaji wa mifugo unaofanywa |
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji wa ndege wafugwao katika ufunguzi wa maonesho ya nne ya ndege wafugwao nchini jijini Dar es salaam. |
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akitembelea mabanda mbalimbali katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni