Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof.Elisante
Ole Gabriel leo amefanya ukaguzi mnada ya Awali wa Shanwa uliopo katika
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa na Mwanuzi katika Halmashauri ya Wilaya ya
Meatu.
Akiongea na Katibu Mkuu, Dkt. Gabriel Bura kutoka Wizarani
ambaye pia ni mmoja wa timu Nzagamba, Dkt. Bura,amemweleza Katibu Mkuu kuwa
tangu wamewasili hapo, kazi zinaenda vizuri bila shida yoyote.
Katibu Mkuu tangu timu Nzagamba imeanza kutekeleza majumu yake,katika
mnada wa Senai timu ilifanikiwa kukusanya jumla ya Tsh.7,028,000/=
ukilinganisha na Tsh.756,000/= zilizokuwa zinakusanywa kabla ya Nzagamba kuanza
kutekeleza Majukumu yake. alisema.
Aidha Bura amesema kuwa wafanyabiashara wameanza kuelewa mabadiliko
ya tozo mpya,isipokuwa bado kuna changamoto chache, baadhi ya wafanyabiashara
wanafanya biashara nje Minada kinyume cha sheria ili kukwepa kwa Makusudi
kulipa tozo zilizowekwe kisheria.
Wakati huo huo baadhi ya wafugaji waliokuwepo katika mnada wa
Shanwa Maswa walitoa baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja
na kupigwa faini pale Ngombe wanapofika pungufu katika mnada wa Kizota au Pugu
hata kama atakuwa amekufa njiani kwa kukanyagwa na wenzake.
Akijibu baadhi ya changamoto zilizotolewa na wafugaji na
Wafanyabiashara hao, Katibu Mkuu Mifugo Prof. Ole Gabriel aliwambia
wafugaji/Wafanyabiashara hao kuwa ni vyema kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa
kwa mujibu wa sheria ili waweze kufanya biashara zao za mifugo bila bugudha
yoyote.
Katika hatua nyingine Dkt. Benezeth Lutege akiwa katika Mnada
wa awali wa Mwanuzi Halmashauri ya Wilaya ya Meatu,amemwambia Katibu Mkuu kuwa
zoezi la ukusanyaji ushuru kwa kutumia tozo mpya liliingia dosari baada ya Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kugoma kukusanya ushuru huo kwa kutumia tozo
mpya kwa kisingizio cha kutokupata Taarifa hizo Mapema.
Mkuu nililazimika kutumia nguvu kuwatangazia wafugaji na
Wafanyabiashara kuwa wanatakiwa kulipa viwango vipya vya tozo vilivyopitishwa
na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwaka huu wa fedha na sio vya Mwaka
jana. ;alisema.
Katibu Mkuu akimsikiliza kwa makini Bw. Adam Noti, Afisa Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya ya MASWA (Aliyenyoosha mkono) |
Katibu Mkuu akiwa na badhi ya Wafugaji na wafanyabiashara wa Mifugo katika Mnada wa Shanwa Halmashauri ya Wilaya ya MASWA. |
Katibu Mkuu Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika Mnada wa Shanwa katika Halmashauri ya Wilaya ya MASWA |
Katibu Mkuu akiongea na baadhi ya wafanyabiashara waliopanga foleni wakisubiri kulipia tozo mbalimbali. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni