Leo Katibu Mkuu wa Uvuvi Dkt. Rashid Tamatama alikwenda
kuangalia utekelezaji wa ujenzi wa vyoo 24 hiyo ikiwa ni katika hatua za utekelezaji wa ahadi za Mh.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina alipotembelea sokoni hapo na kubaini mapungu yaliyopo
ikiwemo.
1. Uchakavu wa majengo
2. Upungufu wa vyoo;
3. Kujaa kwa mchanga katika bahari: na
4. Uchakavuwa jokofu la kuhifadhia samaki
Ambapo alisema kuwa Wizara yake itaingilia kwa kuchukua
hatua za haraka katika hayo na kuagiza mara moja kwa ujenzi wa vyoo 24 ambavyo vitapunguza msongamano
sokoni hapo.
Katibu Mkuu wa Uvuvi, Dkt. Rashidi Tamatamah ametembelea soko la samaki Ferri- Kivukoni kuangalia ujenzi wa vyoo 24 ambavyo vitapunguza msongamano katika soko hilo. |
Katibu Mkuu Uvuvi, akielekea eneo la ujenzi akiambatana na Meneja wa soko Bw. Mkuu Anje |
Katibu Mkuu Uvuvi akiwa katika eneo la Ferry |
Katibu Mkuu akiwa na Meneja wa soko hilo akifafanua jambo sokoni hapo |
Choo ambacho kinatumika kwa sasa na kutokana na wingi wa watu hakikidhi maitaji yao |
Katibu Mkuu akipata maelezo juu ya ujenzi huo unavyoendelea |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni