Wafugaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Hai, Mkoani
Kilimanjaro wamewalalamikia watendaji wa Serikali na kwamba wao ndio wanao chochea Migogoro kati ya Wakulima
na Wafugaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai.
Malalamiko hayo yametolewa jana na wafugaji wa kijiji cha
Sanya Station, katika kata ya Kia, katika Halmashauri ya Wilaya Hai, walipokuwa wakitoa kero zao kwa
Katibu Mkuu Mifugo, Prof.Elisante Ole Gabriel, aliyefika katika kijiji hicho kusikiliza kero za
wafugaji hao kwa Niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe .Luhaga Joelson Mpina.
“Sisi Wafugaji na Wakulima natuna tatizo kabisa, Shida kubwa
iko kwa hao Mgambo, ambao wanatumwa na watendaji wa Serikali waje wakamate Ngombe
wetu bila kosa lolote na kufanya mradi wao wa kuwaingizia fedha;.alisikika
Mfugaji akilalamika.
Aidha watumishi waliopo katika taasisi za Umma za NARCO na
TALIRI ,West Kilimanjaro nao wamelalamikiwa na wafugaji hao kuwa ni vinara wa kuchukua
rushwa hasa Ngombe wa wafugaji wanapokamatwa wakiwa katika maeneo ya Taasisi hizo wakipata
Malisho.
Aidha,Wafugaji wa kijiji cha Sanya Station wamemweleza
katibu Mkuu kuwa, changamoto kubwa waliyonayo kwa sasa katika kijiji hicho ni pamoja na, uhaba
wa maeneo ya Malisho, Mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda wa miaka 30, ambapo mamlaka ya kiwanja cha
ndege ya KIA wananataka kuwapora ardhi waliyoridhishwa na Mababu zao ,Eneo halali
lenye kubwa wa Hekta Elfu 11, lenye wakazi zaidi ya Elfu ishirini na nne (24,000) katika kata ya
Kia.
Changamoto nyingine waliyotaja ni pamoja na ubovu wa
miundombinu ya Majosho ,ukosefu wa visima virefu vya kunyweshea Maji Mifugo na kukosekana kwa Mnada
katika Eneo hilo.
Kwa upande wake Katibu wa chama cha Wafugaji Taifa Bw. Magembe
Makoye, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe John Pombe Magufuli kwa
Kuwateua Viongozi waandamizi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ukianzia na Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Luhaga Joelson Mpina, Katibu Mkuu Mifugo, Prof.Elisante Ole Gabriel ambao kwa asili wote
ni wafugaji.
Makoye amewaasa Wafugaji kufuata kanuni, Taratibu na sheria
za nchi ili waendelee
kuheshimika, kwani wafugaji wanajitosheleza kwa kila kitu
ndio maana hawajawahi kuomba chakula Serikalini na wanasomesha watoto wao bila tatizo lolote.
Tunaomba Serikali ipime maeneo ya wafugaji ili wamilikishwe
kisheria, Sasahivi kila hifadhi
imeanzisha Mahabusu ya Mifugo, Ngombe wakikamatwa ndani ya
hifadhi anapigwa faini ya
Tsh.100,000/= kwa ngombe mmoja. Hii ni rasimu ya sheria
ambayo ilikuja kwa wadau tuliikataa, cha kushangaza watu wa Maliasili wanaitumia, hii ni sheria
kandamizi ;alisema.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Hai Bw.Lengai Ole
Sabaya amepiga Marufuku kwa watendaji wa Vijiji na Vitongoji kupokea fedha yoyote ya Migogoro kati
ya Wakulima na Wafugaji. Mhe Sabaya amesema kuwa Migogoro mingi inayotokea ni kwa sababu
wananchi wa kifugaji hawashirikishwi katika ngazi za maamuzi.
Akifanya Majumuisho ya Mkutano huo, Katibu Mkuu Mifugo Prof.
Elisante Ole Gabriel ameishukuru kamati ya Ulinzi na Usalama ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai
kwa kutatua Migogoro iliyopo kwa Weledi Mkubwa.
Ole Gabriel amesema kuwa Serikali inatambua haki za
Wafugaji,katika nchi hii wafugaji ni
wawekezaji, Lakini ni lazima wafugaji wazingatie sheria, kwani
wanamchango mkubwa sana katika Uchumi wa Viwanda.
Rais Magufuli anawapenda wafugaji lakini pia yeye mwenyewe
ni Mfugaji, ndio maana katika ilani ya Chama cha Mapinduzi Ibara ya 25 yote
inaongelea Wafugaji na namna Bora ya kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Prof.Gabriel amesema kuwa changamoto mbalimbali
walizozieleza Wafugaji hao zinafanyiwa kazi kwani Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. John Joseph
Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Sikivu.
Pia Katibu Mkuu Mifugo aliwakumbusha wafugaji kuachana na
kufuga kwa mazoea, amewambia wakati umefika sasa kubadilika na kuanza kufuga Kisasa na
Kibiashara.
Katibu Mkuu Mifugo na Mbunge wa Siha Dr. Mollel wakifurahia jambo mara baada ya Mzee wa jamii ya kimasai kuja kuwasalimia mara baada ya mkutano kumalizika. |
Katibu Mkuu akiongea na wafugaji |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni