Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2017
Picha
TANZANIA NA UGANDA ZASAINI MAKUBALIANO YA KUBORESHA SEKTA YA MIFUGO Na John Mapepele Tanzania  na Uganda leo zimesaini  makubaliano ya kuboresha sekta ya mifugo baina ya nchi mbili kwa kuimarisha ushirikiano katika nyanja za kuthibiti magonjwa hatari ya mlipuko na kuanzisha minada ya  pamoja ya kimataifa kwa maslahi ya nchi zote mbili. Makubaliano hayo yamesainiwa  kwa upande wa Uganda na Balozi wa Uganda nchini bwana Richard Tumusiime  Kabonero na kwa upande wa Tanzania na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo anayeshughulikia sekta ya Mifugo, Dkt. Mary  Mashingo mjini Bukoba.  Akizungumza mara baada ya utiaji wa saini makubaliano hayo Balozi Kabonero amesema magonjwa ya mlipuko kwa wanyama hayana mipaka hivyo makubaliano yaliyofanyika yatasaidia kudhibiti magonjwa ya wanyama  hatimaye kuboresha  mifugo. Aidha, amesema  hatua  ya udhibiti wa magonjwa ya mifugo itasaidia kupata mifugo bora itakayokuwa na thamani kubwa katika masoko y...

ZIARA YA KATIBU MKUU SEKTA YA MIFUGO DKT. MARIA MASHINGO ALIPOTEMBELEA MKOA WA KAGERA

Picha
Katibu Mkuu waWizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo akiongea na wafugaji wa nchini Uganda katika eneo la Omwaarogwamabaare akiwa na balozi wa Uganda nchini Tanzania Mhe. Richard Tumusiime Kabonero waliomzunguka ni wataalam mbalimbali kutoka Wizarani. Katibu Mkuu waWizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo(aliyeshikafimbo) akipima kina cha Kisima kilitengenezwa kienyeji kwaajili ya kunyweshea mifugo katika eneo la Kafunjo Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera. Waliomzunguka ni wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizaraya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa na Halmashauri ya Missenyi. Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo (aliyenyanyuamkono) akimweleza jambo Balozi wa Uganda nchini Tanzania Mhe. Richard Tumusiime Kabonero walipokuwa katika ziara ya kikazileo kwenye Mto Kagera katikakijiji cha Kakunyu Wengine kushoto k...
Tanzania na Uganda yapiga hatua katika kudhibiti magonjwa ya milipuko Na John Mapepele Balozi wa Uganda nchini Bw Richard Tumusiime Kabonero amesema ushirikiano wa karibu baina ya Tanzania na Uganda kwenye sekta ya mifugo unahitajika ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko ambayo ni hatari kwa mifugo ya pande zote mbili. Akizungumza leo mjini Bukoba kwenye mkutano wa wataalam wa mifugo wa Tanzania na Uganda ulioandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi nchini, Balozi Kabonero amesema njia bora ya kudhibiti magonjwa ya wanyama ni kuwa na timu ya pamoja ya wataalam watakaokuwa wakifuatilia hali ya mifugo na kufanya tathmini kila wakati badala ya utaratibu wa sasa wa kila nchi kushughulikia peke yake. “Uganda kama ndugu wa karibu wa Tanzania tuna kila sababu ya kushirikiana ili kuboresha sekta hii” alisisitiza balozi Kabonero Akizungumzia kwa upande wa Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo anayeshughulikia sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo amewataka wafugaji wa asili kote nchin...
Picha
NAIBU WAZIRI ULEGA AKAMATA TANI 11 ZA SAMAKI WALIOKUWA WAKITOROSHWA BILA KULIPIWA USHURU WA TSH. 99,000,000/= Na Kumbuka Ndatta Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalla Ulega amekamata tani 11 za Samaki aina ya Sangara katika soko la kimataifa la Mwaloni jijini Mwanza waliokuwa wakitoroshwa bila kuliopiwa wa ushuru wa Tsh.99,000,000 kwenda nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hivi karibuni Samaki hao walikuwa wakitoroshwa na wafanyabishara kutoka nchini Kongo waliokuwa na kibali kinachoonyesha   wanaenda kuuzwa Tunduru Mkoani Ruvuma.   “Jamani naomba msimamie sheria ili kulinda rasilimali zetu zisitoroshwe kwenda nje bila kulipiwa kodi. Lazima tumuunge mkono Rais wetu John Pombe Magufuli katika kuhakikisha Rasilimali hizi ziwanufaishe wananchi na sio watu wachache”alisisitiza wakati akiongea na uongozi wa Manispaa ya Ilemela. Ulega amesema kuwa ni kinyume cha sheria kuvua samaki wachanga na wazazi, na ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Ilemel...
Picha
WAZIRI MPINA AFUTA TOZO ZOTE ZA MIFUGO ZISIZOZINGATIA SHERIA. Na John Mapepele Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amefuta tozo ya faini ya shilingi elfu hamsini kwa kila Ng’ombe mmoja na ameuagiza Uongozi wa Wilaya ya Singida kuwarudishia mara moja fedha wafugaji wote  walizotozwa faini kinyume cha Sheria  katika zoezi  la kukamata mifugo linaloendelea katika Hifadhi ya Msitu wa Jamii wa Mgori. Waziri Mpina ametoa maelekezo hayo leo alipotembelea eneo la Hifadhi ya Msitu wa Jamii wa Mgori, kwenye Kijiji cha Handa na kuwaagiza Wakuu wa Mikoa ya Singida na Dodoma kupitia kwa Wakuu wa Wilaya ya Singida na Chemba kushirikiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo kufika katika eneo hilo kabla ya tarehe15/12/2017 kushughulikia mipaka baina eneo la Singida na Handa kwa upande wa Wilaya ya Chemba  na migogoro ya wafugaji inayoendelea. “Kama Waziri mwenye dhamana ya kushughulikia Sekta ya Mifugo na Uvuvi nchini...
Picha
  MPINA AMSIMAMISHA KAZI MTUMISHI ALIYESHIRIKI UTOROSHAJI WA KILO 2500 ZA SAMAKI KWENDA BURUNDI ZENYE THAMANI YA SHILINGI 20,850,000.00 Na   John Mapepele Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina amemuagiza   Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yohana   Budeba kumsimamisha   kazi mara moja Afisa wa Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera bwana   Ayoub Ngoma kwa tuhuma za   kushiriki   katika utoroshaji wa samaki wenye kilo 2530 kwenda nchini Burundi zenye thamani ya shilingi 20,850,000/= hapo jana. Akizungumza katika Ofisi ya Kitengo hicho iliyopo mjini Kagera, Mpina   alisema   mnamo tarehe 03/12/2017 majira ya Saa 03:00   asubuhi, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara ilikamata gari lenye namba za uasajili T 614 CLQ aina ya Mitsubishi Canter likiwa limepakia samaki zenye uzito wa kilo 2,000 aina ya Sangara na kilo 530 wa aina ya Sato kwenye mpaka wa Murusagamba wilayani Ngara. ...
Picha
MPINA ABARIKI NARCO KUVUNJA MKATABA WA MWEKEZAJI MZEMBE KATIKA RANCHI YA KAGOMA Na John Mapepele Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Luhaga Mpina  ameridhia  maamuzi ya Kampuni ya Ranchi za NARCO kuvunja mkataba baina ya mwekezaji Agri Vision Global Ltd katika  Ranchi ya Kagoma  mkoani Kagera na kuamuru aondoka mara moja baada ya mwekezaji huyo kushindwa kutekeleza mkataba huo katika kipindi cha miaka mitano. Waziri Mpina ametoa maelekezo  hayo jana  alipotembelea Ranchi ya Kagoma kuangalia shughuli mbalimbali  katika Ranchi hiyo ambapo ametoa siku saba kwa mwekezaji huyo kuondoka katika eneo hilo na badala yake Serikali kupitia NARCO kuendelea kusimamia shughuli za mifugo katika Ranchi hiyo. “Ninakuagiza  Mkuu wa Wilaya  kuanzia sasa  hakikisha unaimarisha ulinzi katika ranchi hii katika kipindi cha kukabidhi Ranchi baina ya Serikali na Mwekezaji  ili kusitokee hujuma zozote” alisisitiza Mpina Alitaja baadh...
WAZIRI MPINA AUNDA TUME KUCHUNGUZA MKATABA WA KIWANDA CHA NYAMA DODOMA NA SERIKALI. Aagiza Rachi za mifugo kuanza kuchinja mifugo katika kiwanda hicho ifikapo Machi mwakani. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina ameunda tume ya watu watano   kufanya tathmini ya utekelezaji wa mkataba   wa kiwanda cha nyama cha Dodoma baina ya   Serikali na Kampuni ya nyama Tanzania(TMC) baada ya muda wa mkataba wa miaka mitano kuisha huku uzalishaji wake ukiwa unasuasua. Mh. Mpina alitoa maelekezo hayo hivi karibuni   kwa Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, bwana Nashon Kalinga   katika ofisi za kiwanda hicho wakati alipokuwa kwenye ziara ya kukagua shughuli mbalimbali za sekta ya mifugo akitokea katika ranchi ya Kongwa. “Mimi kama Waziri mwenye dhamana ya Mifugo naelekeza kwamba Tume ipitie Mkataba   huu   ambao ushaisha muda wake na ikibainika kuwa wameshindwa kutekeleza nitaamuru kuvunjwa mara moja ili   kiwanda kifanye kazi kama ilivyokusudiwa” al...
Picha
WAZIRI MPINA AAGIZA MIKATABA YA VITALU VYA RANCHI YA TAIFA VYENYE JUMLA YA HEKTA Waziri MPINA 68238 KUVUNJWA MARA MOJA. Waziri wa   Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina ameagiza Mtendaji Mkuu wa Ranchi za   Mifugo za Taifa, Profesa Philemoni Wambura kuvunja   mikataba ya wawekezaji wa vitalu vyenye jumla ya hekta 68,238 kwenye ranchi ya Mkata na Dakawa ndani ya mwezi   mmoja baada kushindwa kuviendeleza vitalu   vya ranchi na kushindwa kulipia kwa muda mrefu. Mpina ameyasema hayo jana wakati alipotembelea katika ranchi ya Mkata na Dakawa kwa lengo la kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika   katika ranchi hizo. Amezitaja kampuni za wawekezaji   ambazo zilizomilikishwa   vitalu zinatakiwa kuvunja mkataba kwa kushindwa kuendeleza upande wa ranchi ya Mkata katika Wilaya ya Kilosa kuwa ni pamoja na Kadolo Farm Company Ltd   kitalu namba 418 yenye hekta 4005,Bagamoyo Farm kitalu namba 419 yenye hekta 3672.96, A to Z Animal Feeds Company Lt...

MHE WAZIRI AMEAGIZA MACHINJIO YA KISASA YA RUVU YALIYOTEKELEZWA KWA MUDA MREFU KUJENGWA NA KUKAMILIKA IFIKAPO DESEMBA, 2018

Picha
Machinjio ya kisasa ya Ruvu lazima yakamilike ifikapo 2018 - Mpina Waziri   wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga   J. Mpina ameagiza machinjio ya kisasa ya Ruvu yaliyotelekezwa kwa muda mrefu kujengwa na   kukamillika   ifikapo Desemba, 2018. Maagizo hayo ameyatoa jana katika ranchi ya Ruvu, alipokuwa katika ziara ya kutembelea baadhi ranchi za mifugo nchini, ambapo amesema ni muhimu machinjio hayo ya ya kisasa yakamilike ili Tanzania ianze kuuza mazao yatokanayo na mifugo katika masoko ya kimataifa. Ametoa siku tatu kwa Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kumpelekea mpango kazi unaoainisha   namna ya kukamilisha ujenzi wa machinjio hiyo ya kisasa ambayo   baada ya kukamilika itakuwa machinjio kubwa kuliko zote nchini. Amesema kuwa Tanzania ni nchi ya tatu katika bara la Afrika kwa kuwa na uwingi wa mifugo hivyo hakuna sababu ya kushindwa kuongoza katika   soko la mazao ya mifugo katika masoko ya duniani. Aidha, Waziri Mpina   amese...

REQUEST FOR EXPRESSIONS OF INTEREST

Picha
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA MINISTRY OF LIVESTOCK AND FISHERIES (FISHERIES) SOUTH WEST INDIAN OCEAN FISHERIES GOVERNANCE AND SHARED GROWTH PROGRAM (SWIOFish) PROJECT- IDA CREDIT No.5589-TZ REQUEST FOR EXPRESSIONS OF INTEREST Assignment Title :   PROVISION OF CONSULTANCY SERVICES TO CONDUCT HOUSEHOLD SURVEYS IN SELECTED COASTAL FISHING COMMUNITIES IN MAINLAND TANZANIA & ZANZIBAR, TO ESTABLISH A BASELINE DATASET FOR ASSESSING IMPACT OF THE SWIOFish PROJECT Reference No. TENDER No. ME/021/2017-18/SWIOFish/C/23 The Government of the United Republic of Tanzania has received financing from the World Bank toward the cost of the South West Indian Ocean Fisheries Governance and Shared Growth program – SWIOFish , and intends to apply part of the proceeds for consulting services. The consulting services (“the Services”) include To establish a statistically robust, representative baseline dataset for indicators relevant to househol...