NAIBU
WAZIRI ULEGA AKAMATA TANI 11 ZA SAMAKI WALIOKUWA WAKITOROSHWA BILA KULIPIWA
USHURU WA TSH. 99,000,000/=
Na
Kumbuka Ndatta
Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalla
Ulega amekamata tani 11 za Samaki aina ya Sangara katika soko la kimataifa la
Mwaloni jijini Mwanza waliokuwa wakitoroshwa bila kuliopiwa wa ushuru wa
Tsh.99,000,000 kwenda nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hivi karibuni
Samaki hao walikuwa
wakitoroshwa na wafanyabishara kutoka nchini Kongo waliokuwa na kibali
kinachoonyesha wanaenda kuuzwa Tunduru
Mkoani Ruvuma.
“Jamani naomba msimamie sheria ili kulinda rasilimali
zetu zisitoroshwe kwenda nje bila kulipiwa kodi. Lazima tumuunge mkono Rais
wetu John Pombe Magufuli katika kuhakikisha Rasilimali hizi ziwanufaishe wananchi
na sio watu wachache”alisisitiza wakati akiongea na uongozi wa Manispaa ya
Ilemela.
Ulega amesema kuwa ni
kinyume cha sheria kuvua samaki wachanga na wazazi, na ameuagiza uongozi wa
Manispaa ya Ilemela kupitia Mkurugenzi wake Bw.John Wanga kusimamia sheria
ipasavyo ili kudhibiti kuvuliwa kwa samaki wasioruhusiwa kisheria.
“Ikitokea wakati wa ukaguzi
wenu mmekamata Samaki wachanga au wazazi taifisheni na sheria ichukue mkondo
wake mara moja kwa yeyote anayehusika au anayevunja sheria kwa kujua au
kutokujua”alisema Ulega.
Akihutubia wafanyabiashara
katika soko la Mwaloni jijini Mwanza, Waziri Ulega alielezwa changamoto
wanazokumbana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maji safi na salama na ubovu
wa miundombinu ya vyoo katika soko hilo.
Mhe.Ulega amempa siku tatu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemele Bw.John Wanga kuhakikisha maji na Miundombinu
ya vyoo sokoni hapo inashughulikiwa ndani ya siku tatu, hadi ifikapo Disemba
18, 2017.
Mhe. Naibu Waziri Abdallah Ulega ashika Tani 11 ya samaki waliokuwa wakitoroshwa bila kulipwa ushuru |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni