MPINA ABARIKI NARCO KUVUNJA MKATABA WA MWEKEZAJI MZEMBE KATIKA
RANCHI YA KAGOMA
Na John Mapepele
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Luhaga Mpina ameridhia maamuzi ya Kampuni ya Ranchi za NARCO kuvunja
mkataba baina ya mwekezaji Agri Vision Global Ltd katika Ranchi ya Kagoma mkoani Kagera na kuamuru aondoka mara moja
baada ya mwekezaji huyo kushindwa kutekeleza mkataba huo katika kipindi cha
miaka mitano.
Waziri Mpina ametoa maelekezo
hayo jana alipotembelea Ranchi ya
Kagoma kuangalia shughuli mbalimbali
katika Ranchi hiyo ambapo ametoa siku saba kwa mwekezaji huyo kuondoka
katika eneo hilo na badala yake Serikali kupitia NARCO kuendelea kusimamia
shughuli za mifugo katika Ranchi hiyo.
“Ninakuagiza Mkuu wa
Wilaya kuanzia sasa hakikisha unaimarisha ulinzi katika ranchi
hii katika kipindi cha kukabidhi Ranchi baina ya Serikali na Mwekezaji ili kusitokee hujuma zozote” alisisitiza
Mpina
Alitaja baadhi ya mambo ambayo hayakutekelezwa na mwekezaji huyo
kuwa ni pamoja na kujenga machinjio ya nyama, kujenga kiwanda, kutoa gawio la shilingi
bilioni tatu kila mwaka katika kipindi cha miaka mitano, kutoa shilingi 2672
kwa hekta moja kama tozo la ardhi na kushindwa kuendeleza miundombinu ya NARCO
waliyoikuta wakati wanaingia mikataba
hiyo miaka mitano iliyopita.
Waziri Mpina amemuagiza
Meneja Mkuu wa NARCO, Profesa Philemoni
Wambura kuhakikisha kwamba ndani ya siku
saba anamleta Meneja katika Ranchi hiyo kwa ajili ya usimamizi wa shughuli za
ranchi hiyo na kuhakikisha kuwa inafanya kazi zake kisasa.
Aidha Mpina ametoa siku saba
kwa Uongozi wa NARCO kuhakikisha
kuwa imefanya tathmini ya hasara
zilizosababishwa na mwekezaji huyo ili taratibu za kisheria zichukuliwe dhidi
yake ili aweze kuilipa Serikali ikiwa ni
pamoja na shilingi bilioni kumi na tano kama
gawio la miaka mitano iliyokaa ambalo amesema halijawahi kulipwa hata
shilingi moja.
“Sasa tumeamua kuchukua hatua na tutaendelea kuchukua hatua kali
dhidi ya wawekezaji wasiowaaminifu wanaotaka kuihujumu serikali katika sekta
hizi za mifugo na Uvuvi” alihoji Mpina
Alionya wawekezaji kuacha tabia ya kuidanganya serikali kwamba
wanauwezo wa kuwekeza katika vitalu ili
wapewe lakini wanabadili matumizi baada ya kupewa. Aliongeza kwamba Serikali imegundua baadhi ya wawekezaji wanaopewa vitalu
wanawakodisha wafugaji kutoka nchi jirani na kujipatia faida wakati Serikali haipati chochote.
Awali, akipewa ripoti ya maendeleo ya mifugo na uvuvi
na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Deodatus Kinawiro mbaye ni Mkuu wa Wilaya ya
Bukoba . alisema kutokana na oparesheni za uvuvi haramu zinazoendelea wilaya ya
ngara imekamata tani 6 za samaki zilizokuwa zikipelekwa katika nchi ya burundi
.
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina
akiwa na viongozi wa Mkoa wa Kagera wa Serikali mara baada ya kuwasili
jana kukagua shughuli za mifugo katika Ranchi za Mifugo zilizopo Mkoani.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni