Nav bar

Jumanne, 5 Desemba 2017

MHE WAZIRI AMEAGIZA MACHINJIO YA KISASA YA RUVU YALIYOTEKELEZWA KWA MUDA MREFU KUJENGWA NA KUKAMILIKA IFIKAPO DESEMBA, 2018


Machinjio ya kisasa ya Ruvu lazima yakamilike ifikapo 2018 - Mpina

Waziri  wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga  J. Mpina ameagiza machinjio ya kisasa ya Ruvu yaliyotelekezwa kwa muda mrefu kujengwa na  kukamillika  ifikapo Desemba, 2018.

Maagizo hayo ameyatoa jana katika ranchi ya Ruvu, alipokuwa katika ziara ya kutembelea baadhi ranchi za mifugo nchini, ambapo amesema ni muhimu machinjio hayo ya ya kisasa yakamilike ili Tanzania ianze kuuza mazao yatokanayo na mifugo katika masoko ya kimataifa.

Ametoa siku tatu kwa Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kumpelekea mpango kazi unaoainisha  namna ya kukamilisha ujenzi wa machinjio hiyo ya kisasa ambayo  baada ya kukamilika itakuwa machinjio kubwa kuliko zote nchini.

Amesema kuwa Tanzania ni nchi ya tatu katika bara la Afrika kwa kuwa na uwingi wa mifugo hivyo hakuna sababu ya kushindwa kuongoza katika  soko la mazao ya mifugo katika masoko ya duniani.

Aidha, Waziri Mpina  amesema  kukamilika kwa machinjio hayo kutasaidia kupunguza  usumbufu kwa wafanyabiashara wa mifugo ambao wote nawapeleka mifugo yao Dar es Salaam   hali ambayo inaongeza uharibifu wa mazingira  kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Waziri Mpina amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Ranchi  za taifa kuhakikisha kuwa  kunatafutwa fedha kwa ajili ya kuzalisha  mbegu bora za mifugo na kuongeza idadi ya mifugo kulingana na uwezo wa eneo la ranchi ya Ruvu lenye ukubwa wa hekta 44,000 ambapo hivi sasa eneo hilo la ranchi ya Ruvu lina mifugo ipatayo 1530 wakati uwezo wa ni kuwa na mifugo kuanzia 12000 hadi 22000.

Alisisitiza kwamba maboresho hayo lazima yafanyike ifikapo Desemba , 2018  ambapo ifikapo Juni 2018 tathimini ya awali itafanyika kuona ni kwa namna gani agizo hilo limetekelezwa.

“Tunataka wananchi wapate sehemu ya kujifunza,ranchi ya Ruvu iwe sehemu ya kupata mbegu bora. Siwezi kuwa Waziri wa Mifugo wakati shamba langu halina mifugo” alisisitiza  Mpina.

Waziri aliongeza kuwa na mfumo wa kisasa wa kufuga  mifugo kitaalamu  badala ya mfumo wa sasa ambapo mifugo  inafugwa  kwa muda mrefu.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akijaribu kukata nyama kwa kutumia mashine ya kisasa alipotembelea ranchi ya Ruv

Jengo la machinjio ya kisasa lililopo katika eneo la ranchi ya Ruvu ambalo Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina amewaagiza Watendaji kuhakikisha linakamilika ifikapo Desemba 2018.

Waziri wa Mifugo na  Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akiwa na  viongozi wa ranchi ya mifugo nchini akionyeshwa mbuzi wanaofugwa katika ranchi ya Ruvu

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akihakiki taarifa za ununuzi wa dawa za mifugo alipotembelea ranchi ya mifugo ya Ruvu hivi karibuni.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ranchi ya Ruvu na watumishi wa Wizara  ya Mifugo na Uvuvi alipotembelea ranchi.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni