WAZIRI MPINA AUNDA TUME KUCHUNGUZA MKATABA WA KIWANDA CHA NYAMA DODOMA NA
SERIKALI.
- Aagiza Rachi za mifugo kuanza kuchinja mifugo katika kiwanda hicho ifikapo Machi mwakani.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga
Mpina ameunda tume ya watu watano
kufanya tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa kiwanda cha nyama cha Dodoma baina ya Serikali na Kampuni ya nyama Tanzania(TMC)
baada ya muda wa mkataba wa miaka mitano kuisha huku uzalishaji wake ukiwa
unasuasua.
Mh. Mpina alitoa maelekezo hayo hivi
karibuni kwa Meneja Mkuu wa Kiwanda
hicho, bwana Nashon Kalinga katika ofisi
za kiwanda hicho wakati alipokuwa kwenye ziara ya kukagua shughuli mbalimbali
za sekta ya mifugo akitokea katika ranchi ya Kongwa.
“Mimi kama Waziri mwenye dhamana ya
Mifugo naelekeza kwamba Tume ipitie Mkataba
huu ambao ushaisha muda wake na ikibainika
kuwa wameshindwa kutekeleza nitaamuru kuvunjwa mara moja ili kiwanda kifanye kazi kama ilivyokusudiwa”
alisisitiza Mpina
Alisema Tume hiyo itawashirikisha
wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Msajili wa
Hazina na Ranchi za Taifa za Mifugo.
Katika hatua nyingine, Mh. Waziri
amesitisha mkutano wa Bodi ya Kiwanda hicho uliotakiwa kufanyika tarehe 8
Disemba mwaka huu hadi Tume hiyo itakapowasilisha ripoti ya tathmini ya
utekelezaji wa mkataba ulioisha wa miaka mitano.
Hata hivyo Mpina amesema Serikali haiwezi kuruhusu kiwanda kufanya
kazi chini ya kiwango wakati kuna
wawekezaji wengi ambao wana nia ya dhati ya kufanya kazi na kwamba
Tanzania bado ina soko kubwa katika mazao ya mifugo duniani kote.
“Ni bahati mbaya sana tunaona kiwanda
kinageuka machinga badala ya kufanya
kazi na kuleta tija katikakuelekea uchumi wa kati wa viwanda hapa nchini. Sisi
kama Serikali hatukubaliani na hili” aliongeza Mh.Waziri.
Aidha amesema imefika wakati mwafaka
sasa kwa Serikali kwa Ranchi zote za
mifugo kuzalisha katika kiwango cha juu
ili kiwanda hicho cha nyama (TMC) kiwe kinachinja mifugo kutoka Ranchi hizo
na kwa kuanzia amesema ranchi ya Ruvu na Kongwa lazima ziendelezwe mara moja ili kutoa mifugo ya kutosha na kuchinjwa katika kiwanda hicho. Katika
uwekezaji huo Serikali ina hisa ya asilimia 41 wakati muwekezaji ana hisa ya
asilimia 51.
“Nasema kuanziamwezi Machi mwakani
nataka tuwe tunachinja mifugo kutoka
katika ranchi zetu. Naamini hili linawezekana kabisa, ni lazima tuanze sasa”
amesisitiza Mh.Mpina.
Akiwa
katika ranchi ya Kongwa ametoa mwaka mmoja kwa uongozi wa ranchi hiyo
kuongeza idadi ya mifugo kutoka 8647 ya sasa hadi kufika 20000 ifikapo Disemba
2018. Eneo la malisho kuwa limesafishwa
kutoka hekta 3000 za sasa hadi kufikia hekta 6000 katika kipindi hicho
hicho.
Alisema Wizara itafanya tathmini ya
utekelezaji wa maagizo hayo baada ya kipindi cha miezi sita ili kuona utekelezaji
wake.Eneo la ranchi ya Kongwa linaukumbwa wa hekta 38000 ambapo ametaka nusu ya hekta hizo kutumika katika uzalishaji
wa malisho na nusu nyingine kwa ajili ya kuhifadhia mifugo hiyo.
Meneja Mkuu wa Ranchi za Mifugo
nchini, Profesa Philemoni Wambura amesema Rachi ya Kongwa uongozi wa rachi hiyo unamalengo ya kuzifanya
ranchi zote nchini kuwa mashamba darasa
ya kuwafundishia wananchi namna bora ya uzalishaji wa malisho na mbegu
bora za mifugo.
Aidha amesema kwa sasa Ranchi ya Kongwa inayozalisha nyama bora duniani
kinachotakiwa ni kuongeza uzalishaji wa nyama hiyo kwa kuwa mahitaji yake ni
makubwa.
“Mh. Waziri tumepokea maelekezo yako
tunaahidi kuzalisha kwa kiwango cha juu ili tujenge uchumi wetu wa viwanda”
ameongeza Profesa.
Profesa amesema kwa sasa kipaombele cha kwanza ni kuhakikisha
kuwa rachi zinazalisha idadi kubwa ya majike
ya mbegu bora na kusambaza kwa wafugaji wote nchini ili kubadili ufugaji
asilia na kwenda katika ufugaji wa kisasa wenye tija.
“Kwa kufanya hivyo tutapata
mbegu bora za mifugo wanaokuwa haraka,
wanaotoa maziwa mengi na wenye kuhimili magonjwa na hiyo yatakuwa mapinduzi
makubwa katika sekta hii nchini”amesisitiza Profesa.
Hata hivyo amesema mpango wa ranchi
ni kuangalia namna bora ya kuziingiza
aina nyingine za ng’ombe kutoa kataika mikoa ya singida(Singida White),
Sumbawanga(Fipa Type) na Iringa(Iringa Red) ili kuboresha zaidi badala ya
kutegemea mbegu kutoka nje ya nchi ambazozina kufa kwa kiasi kikubwa baada zinashindwa kuhimili
hali ya hapa nchini.
Katika hatua nyingine, Mh. Waziri
meuagiza uongozi wa rachi kuangalia namna ambavyo wanaweza kupunguza gharama ya
kuuza mbegu bora za mifugo, ambapo kwa sasa dume la ngombe aina ya Borani
linauzwa kwa milioni mbili hali ambayo inawafanya wafugaji wengi kushindwa
kumudu.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu
aneyesimamia Sekta ya Mifugo katika ziara hiyo, bwana Victor Mwita, amesema kwa
sasa Wizara imejipanga kuhakikisha uzalishaji wa malisho bora unasimamiwa kikamilifu ili mifugo
inayozalishwa kuwa na tija.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni