Machapisho

LITA YATAKIWA KUENDELEA KUTOA MAFUNZO YA MUDA MFUPI KWA WAFUGAJI

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki ameiagiza Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) kuendelea kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa wafugaji ili wafuge kisasa.   Waziri Ndaki ameyasema hayo leo (28.10.2021) alipotembelea Kampasi ya Tengeru iliyopo mkoani Arusha kwa lengo la kufungua bweni la wasichana lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 ambalo litasaidia kupunguza changamoto ya miundombinu iliyopo.   “Wafugaji bado wanahitaji kupatiwa elimu ya ufahamu ili waweze kuelewa faida na hasara za kuendelea na njia ya ufugaji wa asili na njia bora za ufugaji wa kisasa utakaoweza kuwaletea tija ambapo kwa kuwatumia wataalam tunaowafundisha na waliopo katika maeneo mbalimbali tutaweza kubadilisha fikra za wafugaji wetu,” alisema Waziri Ndaki   Pia LITA imetakiwa kusaidia kutatua changamoto ya malisho kwa wafugaji kwa kutoa elimu juu ya umiliki wa maeneo na upandaji malisho. Waziri Ndaki amesema kupitia mashamba yao ya malisho ambayo hutumika kuwafundishia wan...

NDAKI: TUMIENI UTAALAM WENU KUWAELIMISHA WAFUGAJI NA WAVUVI

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amewataka wataalamu wa mifugo na uvuvi kutoa elimu ya kitaalam kwa wafugaji na wavuvi ili waweze kufuga kwa tija.   Waziri Ndaki aliyasema hayo leo (27.10.2021) wakati akifungua Mkutano wa 44 wa Wataalam wa Uzalishaji Mifugo Tanzania (TSAP) wenye kauli mbiu ya Uzalishaji Endelevu wa Mifugo na Samaki wakati wa janga la UVIKO 19 uliofanyika kwenye ukumbi wa Olasiti Garden Hotel jijini Arusha.   Kutokana na janga la UVIKO 19, wataalam wametakiwa kuongeza kasi katika utoaji elimu kwa wafugaji na wavuvi ili kuwapa mbinu bora zitakazowasaidia kuongeza uzalishaji na kuweza kukidhi soko la nyama na samaki ambalo kwa sasa linazidi kukua kutokana na kufunguka kwa masoko ya nje ya nchi kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kufungua fursa za masoko ya mifugo na samaki nchi za nje haswa kwenye masoko ya Uarabuni, Ulaya na China.   Pia amewasihi wataalam walioshiriki mkutano huo kuishauri s...

WAZIRI NDAKI ANG’AKA UKUSANYAJI MDOGO WA MADUHULI*

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb) amewaagiza watendaji wakuu wa wizara kuhakikisha makusanyo ya maduhuli yanafikia malengo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 baada ya kupokea taarifa ya makusanyo ya robo mwaka ya bajeti hiyo ambayo hakuridhika nayo ukilinganisha na bajeti iliyopita. Akizungumza leo (26.10.2021) katika kikao cha kupokea taarifa ya ukusanyaji wa maduhuli ya robo mwaka kwa bajeti ya wizara ya mwaka wa fedha 2021/22 Sekta ya Mifugo jijini Dodoma, Waziri Ndaki amesema utaratibu wa ukusanyaji maduhuli uko wazi lakini kuna shida ya namna ya ukusanyaji pamoja na fedha nyingine kutojulikana zinapopelekwa baada ya kukusanywa. Ameongeza kuwa amesikitishwa na baadhi ya minada ya mifugo, kutofikia malengo yaliyowekwa katika robo ya mwaka ya bajeti kati ya Mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu na kumlazimu kutoa uamuzi wa kuwaondoa baadhi ya wasimamizi wa minada kwenye nafasi zao na wengine kuwaweka katika kipindi cha uangalizi ili kufuatilia utendaji kazi wao ka...

WAZIRI NDAKI ATAKA KUWEKWA VIPAUMBELE ZAIDI KATIKA TASNIA YA MAZIWA

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amesema ni muhimu uwekezaji uwekewe kipaumbele katika sekta za uzalishaji zikiwemo za mifugo na uvuvi ili nchi iweze kuuza maziwa nje ya nchi. Akizungumza (21.10.2021) jijini Dodoma wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utendaji kazi wa Bodi ya Maziwa nchini kwa kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Uvuvi amesema matatizo mengi yanaweza kutatuliwa katika tasnia ya maziwa na uzalishaji wa tasnia hiyo ili kukuza wigo wa upatikanji wa kutosha wa maziwa katika ngazi ya uzalishaji. “Suala hili la uwekezaji linapokuwa dogo linatuathiri katika maeneo mengi, kwa kweli unahitajika uwekezaji wa kutosha katika tasnia ya maziwa ili kuongeza uzalishaji na kuweza kuuza maziwa nje ya nchi.” Amesema Mhe. ndaki Aidha amesema serikali imekuwa ikihimiza wafugaji kuwa katika vyama vya ushirika kama nyenzo ya kuweza kuwafikia wafugaji kwa uhakika ili kuzalisha na kukusanya maziwa katika mfumo rasmi kwa ajili ya kutumika katika viwanda vya kuchakata ...

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA, YABAINIKA SEKTA KUKUA

Picha
Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta hiyo ambapo wafugaji wameshauriwa kuwa muda huu ni mzuri kwa wao kuvuna na kuuza mifugo yao. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amebainisha hayo leo (20.10.2021) jijini Dodoma, mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utendaji kazi wa Bodi ya Nyama nchini mbele ya kamati hiyo. Mhe. Ulega amesema kipindi cha nyuma wafugaji walikuwa wakilalamika kutopata masoko ya mifugo yao ila katika kipindi cha sasa uhitaji wa mifugo katika viwanda vya kuchakata nyama nchini umekuwa mkubwa pamoja na hitaji la nyama katika soko la ndani. “Sekta ambayo ulikuwa hauwezi kuisikia inasemwa, lakini leo inakuwa mjadala hivyo ni wakati mzuri sana kwa wafugaji kuvuna na kuuza mifugo yao.” Amesema Mhe. Ulega Amesema serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Ha...

ULEGA: TUMEJIPANGA KUINUA BIASHARA YA DAGAA WA KIGOMA

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imejipanga kuhakikisha Dagaa wa Kigoma wanakuwa ni zao la kimkakati kibiashara litakalokwenda kuvutia uwekezaji na kusisimua uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla. Ulega aliyasema hayo wakati akiongea na Wadau wa Uvuvi alipofanya kikao nao katika Mwalo wa Katonga uliopo Mkoani Kigoma Oktoba 17, 2021. Alisema kuwa serikali imejipanga kufanya zao la dagaa wa Kigoma kuwa la kimkakati kwa sababu biashara ya dagaa inahusisha watu wengi katika jamii, hivyo kuiimarisha biashara hiyo ni kuwaimarisha wananchi kiuchumi. "Sisi Serikali tunataka kuinua biashara ya dagaa wa Kigoma, tunataka wavuvi wainuke kiuchumi, na tumejipanga kuondoa vikwazo vyote vinavyowasumbua na tutalitangaza vyema zao hili ili kuvutia uwekezaji zaidi hapa Kigoma," alisema Ulega Pia, Naibu Waziri Ulega aliwataka Viongozi wa Mkoa huo kuanza mikakati na kampeni maalum kwa...

WAVUVI WAHIMIZWA KUTUNZA MAZALIA YA SAMAKI KUINUA UZALISHAJI

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka wavuvi wanaofanya shughuli zao Wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma kutunza mazalia ya Samaki ili waweze kuzaliana na kuongezeka jambo ambalo litasaidia kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa buluu nchini. Ulega alitoa wito huo wakati akiongea na wavuvi wa Vijiji vya Buhingu  na Igalula alipofanya ziara  ya kukagua shughuli za uvuvi zinazofanyika Mkoani humo Oktoba 16, 2021. Alisema ni muhimu kutunza mazalia hayo kwani ndio kiwanda cha kuzalisha malighafi huku akiwakumbusha wananchi kuwa kwa kufanya hivyo kutapelekea samaki kuongezeka na hivyo watakuwa na uhakika wa kupata lishe bora na kukuza kipato chao. "Wananchi ungeni mkono jitihada za Serikali na wadau wengine wa maendeleo katika kuhakikisha mazingira ya mazalia ya Samaki yanatunzwa vizuri, mkifanya hivyo mazao mengi yatapatikana na uchumi wenu hapa utainuka," alisema Ulega Aliendelea kusema kuwa uchumi wa wananchi hao ukiinuka kupitia biashara nzuri ya sa...