SILINDE AWATAHADHARISHA WAKULIMA, WAFUGAJI, WAVUVI DHIDI YA EL NINO
◼️Aonya mzaha kuhusu uwepo wa mvua hizo
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe, David Silinde amewataka wakulima, wafugaji na wavuvi kuchukua tahadhari dhidi ya Mvua za El Nino.
Mhe.Silinde ametoa tahadhari hiyo Oktoba 12,2026 wakati akifungua Maonesho ya Wiki ya chakula Duniani ambayo yanafanyika kitaifa mkoani Tanga ambapo amewataka wakulima kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu taarifa za namna ya kuendesha shughuli zao bila kuathiriwa na Mvua hizo huku akiwataka wafugaji kujiandaa na namna ya kukabiliana na magonjwa ya Mifugo yanayoweza kuwepo kutokana na mvua hizo.
“Kwa Wavuvi kwa kuwa ndo hasa wanaoweza kuathiriwa zaidi kutokana na shughuli zao kufanyika maeneo ya majini wanatakiwa kufuatilia taarifa za hali ya hewa kabla ya kuelekea kwenye shughuli zao”Ameongeza Mhe. Silinde.
Wakati huo huo Mhe. Silinde amewaonya wananchi wanaopuuza uwepo wa mvua hizo ambapo amesisitiza kuwa taarifa za uwepo wake zimetokana na utafiti wa kisayansi hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuchukua tahadhari hata kama hazitokuwepo.
“Sisi kama Serikali tunatimiza wajibu wetu kwa wananchi kwa kutoa taarifa na kuwataka wachukue wananchi hivyo hata hiyo Elnino isipokuwepo tutamshukuru Mungu kwa sababu hakuna ambaye anataka madhara ya aina hiyo yatokee hapa kwetu na kimsingi tunapaswa kuomba yasitokee” Amesisitiza Mhe. Silinde.
Akisoma taarifa ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Sebastian Shilangalila amesema kuwa Wizara yake imeendelea kuimarisha uzalishaji na tija kupitia uboreshaji wa Mifugo, huduma za afya ya Mifugo, lishe bora ya Mifugo na uzalishaji wa malisho.
“Aidha Serikali inaendelea kusimamia rasilimali za Uvuvi kwa kuzingatia misingi endelevu huku ikiweka mkazo katika kuongeza uzalishaji, tija na kipato cha wananchi wanaojishughulisha na Uvuvi na Ukuzaji viumbe maji.
Wiki ya Chakula duniani inatarajiwa kuendelea mkoani Tanga hadi Oktoba 16,2026 ambapo hulenga kuhamasisha wananchi matumizi ya mlo kamili ili kuondokana na changamoto ya udumavu na utapiamlo.









Maoni
Chapisha Maoni