KIKAO CHA VIONGOZI WA WIZARA NA TAASISI ZAKE CHAHITIMISHWA KIBAHA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amefunga  Kikao cha Viongozi wa Wizara na Taasisi zake kilicholenga kutathimini utendaji kazi wao wa kila siku, kujadili mikakati ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2050 kwa sekta za Mifugo na Uvuvi ngazi ya Wizara na taasisi zake.

Kikao kazi hicho kimefanyika kwa siku tatu katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha Mkoani Pwani, kuanzia  Oktoba 10 hadi 12, 2026, ambapo Viongozi wa Wizara na Taasisi zake walipata nafasi ya kuwasilisha mikakati ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika sekta za mifugo na uvuvi kupitia wizara na taasisi zake.

Aidha, katika Kikao hicho Viongozi hao wa Wizara na Taasiai zake walipata fursa ya mafunzo  elekezi katika masuala mbalimbali ya uongozi lengo ni kuongeza maarifa ya utendaji kazi.

Akifunga Kikao hicho leo Oktoba 12, 2026  Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa pamoja na maagizo yake mengine  amesisitiza  kukamilishwa kwa taratibu za uendeshaji wa Bandari ya Uvuvi, Kilwa pamoja na Meli za Uvuvi wa Bahari Kuu, kufanya kazi pamoja kwa wizara na taasisi zake, Mipango mizuri na Uratibu wa masuala mbalimbali kuhusu uendeshaji wa shughuli za wizara na taasisi zake ili kuleta mageuzi ya sekta.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng'wasi Kamani amesema kikao hicho kiwakumbushe viongozi hao kuwajibika katika kuitumikia serikalikatika, huku Katibu Mkuu wa Wizara Bi. Agnes Meena akiwasisitiza watendaji hao kuhakikisha mikakati ya Wizara na taasisi iakisi Dira ya Taifa Maendeleo ya 2050.










Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TANZANIA DAIRY BOARD

SHAMBA LA KITULO KUWA KITOVU CHA NG’OMBE BORA WA MAZIWA NCHINI

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI