KAMATI YA KUDUMU YA UCHUMI NA UWEKEZAJI YA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR YATEMBELEA FETA
Kamati ya Kudumu ya Uchumi na Uwekezaji ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Mhe Makame Mohammed Sufiani yatembelea Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na FETA katika utoaji wa mafunzo ya Uvuvi.
Kamati hiyo imetembelea FETA kampasi ya Mbegani Tar 24 Oktoba, 2026 na kupokelewa na Mtendaji Mkuu wa FETA Dkt.Semvua Mzighani ambapo aliwapa taarifa fupi ya chuo cha FETA toka kilipoanzishwa mpaka sasa na kuwatembeza katika idara za Ukuzaji viumbe maji pamoja na Uvuvi na Ubaharia.
Akieleza lengo la ziara hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa buluu na Uvuvi Zanzibar, Kapteni Hamad Bakari Hamad amesema kuwa wameamua kuja kutembelea FETA sababu Serikali ya Zanzibar inampango wa kuanzisha Chuo cha Uvuvi hivyo wamekuja FETA kujifunza na kujua mambo muhimu ya kuzingatia kabla hawajaanzisha chuo hiko.
Ameongeza kuwa Watumishi wengi wa Wizara hiyo kule Zanzibar walipatiwa mafunzo yao FETA hivyo wanaamini FETA ni sehemu sahihi zaidi ya kujifunza na kupata matokeo mazuri yakakayowawezesha kuanzisha chuo bora cha Uvuvi.
Naye Mtendaji Mkuu wa FETA Dkt.Semvua Mzighani amewapa taarifa fupi ya Chuo cha FETA tangu kilipoanzishwa mpaka sasa, amewaonesha changamoto mbalimbali zilizopo kwenye sekta hii na namna ya kukabiliana nazo na kuwahakikishia kuwa yupo tayari kutoa Ushirikiano wowote utakaohitajika na Serikali ya Zanzibar kukamilisha adhma yao ya kuanzisha chuo cha uvuvi.








Maoni
Chapisha Maoni