FETA YAENDESHA MAFUNZO YA MATENGENEZO NA UTUNZAJI WA BOTI NA INJINI ZA UVUVI MKOANI LINDI

Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kwa ufadhili wa Mradi wa kukuza Usimamizi Endelevu wa Uvuvi na Ukuzaji viumbemaji Bahari Tanzania (TASFAM) imeendesha mafunzo ya Matengenezo na Utunzaji wa Boti na Injini kwa Maafisa Uvuvi na wavuvi  wanufaika wa mkopo wenye masharti nafuu wa boti za kisasa za uvuvi zilizotolewa na Serikali.

Mafunzo hayo yamehusisha washiriki 20 ambao ni Maafisa Uvuvi wa Wilaya watatu (3) na wavuvi 17 kutoka wilaya tatu za Mkoa wa Lindi Manispaa ya Lindi, Mtama na Kilwa.

Mafunzo hayo ya siku 4 yalianza tarehe15 hadi 18 Oktoba 2026 katika ukumbi wa Chuo cha maendeleo ya wananchi (FDC) Kilwa Masoko Mkoani Lindi.

Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa Bw Shija Lusendamila Lyella amewaasa wahitimu wa mafunzo kutumia ujuzi walioupata kuboresha shughuli zao za uvuvi na kusambaza elimu kwa wavuvi wengine ambao hawakubahatika kupata mafunzo haya.

Washiriki wa mafunzo haya wameishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuiwezesha FETA kupitia mradi wa TASFAM kuwaletea mafunzo haya adhimu ambayo yamewapa uelewa wa namna ya kutunza na kutengeneza  boti na injini ambayo yanaenda kuwa chachu ya mafanikio kwenye utekelezaji wa majukumu yao kwa usalama na tija.









Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TANZANIA DAIRY BOARD

SHAMBA LA KITULO KUWA KITOVU CHA NG’OMBE BORA WA MAZIWA NCHINI

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI