DKT. MADELE ATOA MAELEKEZO KWA WATAALAMU WA MIFUGO ILI KUIMARISHA SEKTA YA MIFUGO
Na. Martha Mbena. Dodoma
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Fabian Madele amewataka wataalamu wa Idara ya Huduma za Mifugo (DVS) kuimarisha utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingatia ufanisi, umoja na ushirikiano, huku wakihakikisha shughuli za sekta ya mifugo zinaendelea kuchangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi wa Taifa. Maelekezo hayo yametolewa Oktoba 08,2026 kwenye kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Wizara hiyo Mtumba, Dodoma.
Dkt. Madele amesisitiza umuhimu wa (open door policy),akieleza kuwa watendaji wanapaswa kuwa tayari kusikiliza changamoto, mawazo na ushauri kutoka kwa wadau na kutafuta suluhisho kwa wakati ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Idara.
“Nasisitiza umuhimu wa ushirikiano na kufanya kazi kama timu (teamwork), kila mtendaji ana nafasi muhimu katika kufanikisha malengo ya Idara, ushirikiano baina ya vitengo na watendaji utasaidia kuongeza ufanisi na kuleta matokeo bora katika huduma za mifugo”. Amesema Dkt. Madele
Aidha, Dkt. Madele ameelekeza umuhimu wa kutumia mfumo wa (feed forward)ambapo maelekezo na taarifa zinazohusu utekelezaji wa majukumu zinapaswa kufikishwa kwa wakati ili kurahisisha ufuatiliaji na kuhakikisha maamuzi yanayofanyika yanaelekezwa katika kuboresha huduma za mifugo nchini.
Katika kikao hicho, Idara ya Huduma za Mifugo, iliwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa majukumu na mwenendo wa shughuli za Idara hiyo, huku idara hiyo ikisisitizwa umuhimu wa kuhakikisha majukumu yaliyopangwa yanatekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia matokeo yanayotarajiwa.



Maoni
Chapisha Maoni