DKT. BASHIRU AWAONDOLEA WAFANYABIASHARA KIKWAZO CHA KUSAFIRISHA MIFUGO

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amewaondolea masharti Wafanyabiashara wanaosafirisha Mifugo nchini ya kulazimika kuwa na  Barua ya Kisheria kutoka kwa Mmiliki wa Leseni ili kisafirisha mifugo yao, na badala yake wataendelea kutumia Vibali vya kusafirishia Mifugo ili kuimarisha biashara hiyo na kuongeza tija na uzalishaji.

Agizo hilo Amelitoa leo Tarehe 7, Oktoba 2026, Jijini Dar es Salaam, Wakati akizungumza na Wadau wa Mnada wa Upili wa Pugu ambapo pamoja na mambo mengine amesikiliza kero na changamoto zinazowakabili wafanyabiashia.

Aidha, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amepiga Marufuku uuzaji holelela wa Mifugo na  Mazao yake ikiwemo, masoko na minada bubu, ambapo ameziagiza Bodi ya Nyama na Maziwa kufanya tathmini ya watu wanaofanya biashara hiyo kiholela kuwafungia  ili kulinda biashara hiyo, na afya za walaji.

Katika Hatua nyingine amemwagiza Mkuruguzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) Kushirikiana na uongozi wa mnada huo, Mkurugenzi wa Jiji kuwapatia maji ya uhakika wafanyabisha, wadau wa mnada wa pugu na wananchi wanaozunguka eneo la mnada ili kuwaondolea adha ya maji wanayokumbana nayo kwa sasa.

Nao baadhi ya wadau wa mnada huo ambao ni wafanyabiashara walieleza changamoto zao zinazo wakabili katika mnada huo ikiwemo ukosefu maji, uwepo wa minada bubu  ya Mbuzi na Kondoo ambayo inasababisha baadhi ya watu kutoingiza mifugo katika eneo la mnada, uvamizi wa eneo la mnada ambapo Waziri alitoa maagizo  ili kutatua changamoto hizo.









Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TANZANIA DAIRY BOARD

SHAMBA LA KITULO KUWA KITOVU CHA NG’OMBE BORA WA MAZIWA NCHINI

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI