DKT. BASHIRU ASISITIZA UMUHIMU WA KUIMARISHA MAWASILIANO KATIKA KUKABILI EL NIÑO
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha mawasiliano na ushirikiano miongoni mwa wadau katika kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu athari za mvua kubwa zinazoweza kusababishwa na hali ya hewa ya El Niño, hususan katika sekta ya mifugo na uvuvi.
Amesema hayo leo, Oktoba 14, 2026, jijini Dodoma, wakati akihitimisha kikao cha tathmini ya awamu ya kwanza na maandalizi ya awamu ya pili ya Mpango wa Kampeni ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo Kitaifa.
Dkt. Bashiru ameeleza kuwa mawasiliano yenye ufanisi ni muhimu katika kuhakikisha taarifa sahihi zinawafikia wafugaji na wadau kwa wakati, hatua itakayosaidia kuongeza uelewa na kuimarisha maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Fabian Magawa Madele ameelezea athari zinazoweza kujitokeza katika Sekta ya Mifugo kutokana na mvua za el nino ikiwemo milipuko ya magonjwa hasa bonde la ufa na homa ya mapafu, vifo vya mifugo, Mifugo kusombwa na maji kutokana na mvua kuwa nyingi na mafuriko, uharibifu wa miundombinu mbalimbali ikiwemo marambo, minada, mabwawa na majosho ya Mifugo pamoja na uhaba wa malisho ya Mifugo na changamoto zabei za bidhaa za Mifugo kushuka.
Pia, Dkt. Madele amesisitiza hatua za kuchukua katika kukabiliana na mvua za el nino ikiwemo kutoa elimu na tahadhari kwa wafugaji, kuchanja Mifugo dhidi ya magonjwa, kuwahamisha mafugaji kutoka maeneo ya bondeni, kuimarisha mabanda ya Mifugo na kuwaelimisha wafugaji umuhimu wa kupunguza idadi ya Mifugo kwa hiari kwa kuwauza kwa wakati.





Maoni
Chapisha Maoni