𝐂-𝐒𝐃𝐓𝐏 𝐘𝐀𝐖𝐄𝐊𝐀 𝐌𝐈𝐏𝐀𝐍𝐆𝐎 𝐌𝐀𝐃𝐇𝐔𝐁𝐔𝐓𝐈 𝐘𝐀 𝐁𝐈𝐌𝐀 𝐊𝐔𝐋𝐈𝐍𝐃𝐀 𝐍𝐆’𝐎𝐌𝐁𝐄 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐔𝐅𝐀𝐈𝐊𝐀
Katika kuhakikisha ng’ombe watakaotolewa kwa wanufaika wa Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP) wanalindwa dhidi ya vihatarishi mbalimbali, Mradi umefanya kikaokazi cha wataalamu kwa ajili ya kupitia na kuboresha mpango wa bima ya mifugo ili kulinda uwekezaji, kupunguza athari za hasara kwa wafugaji na kuimarisha uendelevu wa tasnia ya maziwa.
Kikaokazi hiki cha siku mbili kimeanza leo, Oktoba 22, 2026 na kuwakutanisha maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na mradi wa C-SDTP pamoja na wataalamu wa bima ya mifugo kujadili na kutoa mapendekezo ya kitaalamu kuhusu mpango wa bima kwa ng’ombe watakaotolewa kwa wanufaika wa Mradi Tanzania Bara na Zanzibar.
Wataalam hao wamepitia kwa kina wigo wa bima, masharti na huduma zinazopendekezwa, na kutoa maoni ya kuboresha mpango huo ili kuhakikisha unakidhi mahitaji ya wafugaji na kutoa ulinzi stahiki dhidi ya vihatarishi vinavyoweza kuathiri mifugo yao.
Akizungumza katika kikaokazi hicho, 𝐌𝐫𝐚𝐭𝐢𝐛𝐮 𝐰𝐚 𝐌𝐫𝐚𝐝𝐢 𝐰𝐚 𝐂-𝐒𝐃𝐓𝐏, 𝐃𝐤𝐭. 𝐋𝐚𝐳𝐚𝐫𝐨 𝐊𝐚𝐩𝐞𝐥𝐥𝐚, amesisitiza umuhimu wa kuwapatia wafugaji elimu ya kutosha kuhusu bima ya mifugo, hususan huduma zinazotolewa, vihatarishi vinavyogharamiwa na masharti ya bima, ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi na kuhakikisha ulinzi endelevu wa mifugo yao.


Maoni
Chapisha Maoni