TALIRI YAKABIDHIWA JENGO LA MIKUTANO LA WADAU WA MIFUGO

Na. Stanley Brayton, WMUV

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) imekabidhiwa Rasmi Jengo la Mikutano la wadau wa Mifugo, Jengo ambalo litatumika kuhaulisha teknolojia zitokanazo na Utafiti kwa wadau mbalimbali wa Sekta hiyo wakiwemo Maafisa Mifugo, Wafugaji, Watafiti wa Mifugo na wadau wengine katika kufanya shughuli za Maendeleo ya Mifugo.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo Aprili 13, 2026 Jijini Tanga wakati wa kukabidhiwa Jengo hilo, Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani Wizara ya Mifugo na Uvuvi (DRTE), Ndg. Samwel Mdachi amesema Jengo hilo limejengwa kwa Ufadhili wa Mradi wa Maziwa Faida ambao unatekelezwa na TALIRI pamoja Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA).

"Huu Mradi ni Ufadhili kutoka nchi ya Ireland kupitia Taasisi za Utafiti na Mafunzo TEAGASC., ambao umewalenga wafugaji wa ng'ombe wa Maziwa wa Kanda ya Mashariki ikiwemo wafugaji wa Mkoa wa Tanga, Morogoro, Dar es Salaam, Pwani na mikoa mingine" amesema Ndg. Mdachi

Aidha, Ndg. Mdachi hii yote ni Matokeo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwathamini wafugaji na kutafuta fedha kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo nchini ikiwemo Mradi wa Maziwa Faida unaotekelezwa katika Wilaya ya Muheza.

Vilevile, Ndg. Mdachi amebainisha kuwa Jitihada za Mheshimiwa Rais ndio zimepelekea kujengwa kwa Jengo la Ukumbi wa Mikutano ambalo litatumika na wadau mbalimbali katika kujifunza na kubadilisha uzoefu wa Ufugaji kutokana na mabadiliko na Ukuaji wa teknolojia ya ufugaji.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Prof. Erick Komba amesema tija itakayopatikana kutokana na Matumizi ya Jengo hilo la Mikutano ni pamoja na wadau Mifugo kupata elimu ya Teknolojia mbalimbali za Mifugo ambapo wataenda kuzituma teknolojia hizo katika kuboresha Ufugaji na kuzalisha kwa wingi Mifugo na Maziwa Bora kwa tija.

Pia, Prof. Komba amebainisha majukumu ya TALIRI, yakiwa ni pamoja na kusambaza teknolojia, ambapo kuanzia kwenye kuzibaini, kuzitathimin na kusambaza kwa wadau wa Sekta, na teknolojia za Mifugo zinalenga zaidi kwenye kuongeza Uzalishaji, ustahimilivu wa Mifugo, na kwa sasa TALIRI ina teknolojia nyingi ambazo zinafanyiwa Utafiti na zinalenga kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Naye, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Kanda ya Mashariki - Tanga, Dkt. Zabron Nziku amesema kupitia Mradi huo wa Maziwa Faida, TALIRI imefanikiwa kutathimini na kujiridhiza pasipo shaka Malisho Bora yanayofaa ukanda wa pwani kwa ajili ya ufugaji wa ng'ombe wa Maziwa ambayo yanatambulika kama nyakabindu ambalo sio jina Rasmi ila kwa lugha ya kigeni yanaitwa Cenchrus Ciliaris, na hii teknolojia imeanza kusambazwa kwa wafugaji wa ng'ombe wa Maziwa.

Dkt. Nziku amewaweka wazi wafugaji kuwa ng'ombe Bora ni Malisho na sio Bora Malisho, kwani Malisho Bora yamepatikana ambayo yana vumilia ukame na yana viini lishe muhimu ambavyo vinamuwezesha ng'ombe kutoa Maziwa mengi na yenye ubora.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambaye ni Mkurugenzi Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani (DRTE), Bw. Samwel Mdachi, akizungumza na Maafisa wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), baada ya kuwasili kwa Ziara ya kikazi katika Ofisi za TALIRI Kanda ya Mashariki, Aprili 13, 2026 Tanga.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambaye ni Mkurugenzi Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani (DRTE), Bw. Samwel Mdachi (wa sita kushoto), akisalimiana na Maafisa wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), baada ya kuwasili kwa Ziara ya kikazi katika Ofisi za TALIRI Kanda ya Mashariki, Aprili 13, 2026 Tanga.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Prof. Erick Komba (aliyesimama), akitoa Taarifa ya Taasisi kuhusu Maendeleo ya Utafiti wa Mifugo, wakati wa Kikao kifupi cha kusikiliza Maendeleo ya Mradi wa Maziwa Faida, kilichofanyika katika Ofisi za TALIRI Kanda ya Mashariki, Aprili 13, 2026 Tanga.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Kanda ya Mashariki - Tanga, Dkt. Zabron Nziku, akielezea Maendeleo ya Mradi wa Maziwa Faida, wakati wa Kikao kifupi cha kusikiliza Maendeleo ya Mradi huo, kilichofanyika katika Ofisi za TALIRI Kanda ya Mashariki, Aprili 13, 2026 Tanga.

Mwakilishi wa Meneja Mradi uwa Ujenzi wa Ukumbi wa Mikutano ya Wadau wa Mifugo, ambaye ni Mhandisi Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Lukelo Mgihilwa (aliyesimama), akitoa ripoti ya Mradi wa Ukumbi huo, wakati wa Kikao kifupi cha kusikiliza Maendeleo ya Mradi huo na Makabidhiano ya Mradi, kilichofanyika katika Ofisi za TALIRI Kanda ya Mashariki, Aprili 13, 2026 Tanga.

Picha ni baadhi ya Maafisa wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) wakimsikiliza Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambaye ni Mkurugenzi Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani (DRTE), Bw. Samwel Mdachi, baada ya kuwasili kwa Ziara ya kikazi katika Ofisi hizo za Kanda ya Mashariki, Aprili 13, 2026 Tanga.

Picha ni muonekano wa Ukumbi wa wadau wa Mifugo ambao umejengwa kwa Ufadhili wa Mradi wa Maziwa Faida, uliyopo katika Ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Kanda ya Mashariki, Aprili 13, 2026 Tanga.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambaye ni Mkurugenzi Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani (DRTE), Bw. Samwel Mdachi (mstari wa mbele katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Mifugo na Maafisa wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), wakati wa Ziara ya kikazi katika Ofisi za TALIRI Kanda ya Mashariki, Aprili 13, 2026 Tanga.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO