Nav bar

Jumatano, 1 Oktoba 2025

BI MEENA ATUMA UJUMBE KAMBI YA SHIMIWI MWANZA

◼️Aahidi kutoa kilo 100 za samaki, Ndizi na Viazi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena amewataka wachezaji  wa Wizara hiyo wanaoshiriki michezo mbalimbali kwenye michuano ya SHIMIWI 2025 inayoendelea jijini Mwanza kuendelea kupambana kwa nguvu zao zote huku akiwahakikishia kuwa uongozi wote wa Wizara yake upo pamoja nao.

Bi. Meena amefikisha ujumbe wake kupitia kwa Mkurugenzi wa Uvuvi nchini Prof. Mohammed Sheikh aliyefika kambini hapo kuangalia hali ya maandalizi ya michezo inayofuata inavyoendelea.

“Katibu Mkuu anawapongeza sana na kwa kweli viongozi wote wa Wizara tunafurahishwa sana na maendeleo yenu kwenye michezo mbalimbali mnayoshiriki na hasa mlivyotuheshimisha mbele ya Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Biteko” Amesema Prof. Sheikh.

Aidha Prof. Sheikh amewataka wanamichezo hao kuendelea kuwa wazalendo na kuendeleza jitihada hizo hata baada ya mashindano hayo kumalizika.

Tangu kuanza kwa michuano hiyo Uongozi wa Wizara na Taasisi zake umekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi zinazooneshwa na wachezaji wa Wizara hiyo kwenye michezo mbalimbali wanayoshiriki.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni