Nav bar

Jumatano, 1 Oktoba 2025

KAMBA WANAUME WATINGA NUSU FAINALI SHIMIWI 2025

◼️Sasa kukutana na Ofisi ya Rais-Ikulu

Timu ya mchezo wa kuvuta kamba (wanaume) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya SHIMIWI inayoendelea jijini Mwanza baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mivuto yote miwili dhidi ya timu ya Waziri Mkuu (Sera) kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Katika mchezo huo timu ya Waziri Mkuu (Sera) ilikuwa imedhamiria kuvunja ya kushinda mchezo huo lakini uimara wa wachezaji wa timu ya Mifugo na Uvuvi na matumizi makubwa ya mbinu waliyokuwa nayo viliwafanya kuibuka na ushindi na kufuzu hatua hiyo.

Kufuatia ushindi huo, timu ya Mifugo na Uvuvi inatarajia kucheza na mabingwa watetezi wa michuano hiyo (timu ya Ofisi ya Rais-Ikulu ambao pia ndo mabingwa mara nyingi zaidi wa michuano hiyo tangu iliporejea tena.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni