Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akishuhudiwa na Balozi Ireland Tanzania
Mhe. Mary O’Neill amezindua miundombinu iliyojengwa kupitia mradi wa maziwa
faida unaotekelezwa na kituo cha TALIRI Tanga kwa udhamini wa ubalozi wa Ireland
chini ya Taasisi ya Teagacs.
Akiongea katika uzinduzi
huo Shemdoe amesema Mradi wa maziwa faida mbali na kuboresha miundombinu
mbalimbali lakini pia umekiwezesha kituo hicho kupata vifaa bora vya maabara
kwa ajili ya kufanyia tafiti mbalimbali za mifugo na malisho bora.
Shemdoe ameendelea kueleza
kuwa lengo la mradi wa maziwa faida ambao umegharimu zaidi ya Bilioni 7 ni
kuboresha mnyororo wa thamani wa maziwa kwa wafugaji ambapo kituo cha TALIRI
Tanga kimekuwa kikiendelea kutoa mafunzo kwa vitendo juu ya ufugaji wenye tija
sambamba na kufanya tafiti mbalimbali za mifugo.
Sambamba na hayo, Shemdoe
ametoa wito kwa jamii kuendelea kuzalisha na kutumia maziwa kwa wingi kwani
tafiti zinaonesha kuwa watanzania tunapaswa kutumia lita 200 za maziwa kwa
mwaka lakini ni kiasi cha lita 50 pekee kinatumika kwa kunywa kwa mwaka kwa
watanzania wote.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Prof. Erick Komba
akimshukuru Rais wa awamu ya sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha
mahusiano ya kidemokrasia yaliyopelekea uwepo wa mradi huu muhimu kwa Taifa
wenye kuongeza tija kwa wafugaji amesema TALIRI imejipanga vyema kuhakikisha
mradi wa maziwa faida unaleta manufaa kwa wafugaji na watumiaji wa mazao ya
mifugo.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Kanda ya Mashariki, TALIRI Tanga Dkt. Zabroni Nziku akielezea mafanikio ya
mradi wa maziwa faida amesema Kituo cha TALIRI Tanga kimefanikiwa kutathmini na
kujua aina ya malisho bora, kuendelea kufanya tafiti za kupata ng’ombe bora,
kuanzisha shamba la mfano la malisho, kuwajengea uwezo watafiti, maafisa ugani
na wafugaji ambapo wadau zaidi ya 1000 wamefikiwa na kupatiwa elimu ya ufugaji
bora.
Nae balozi wa Ireland
Tanzania Mhe. Mary O’Neill ameipongeza TALIRI Tanga kwa namna inavyoendesha
mradi huo na kuweza kufikia wadau wengi hususani wafugaji kitendo ambacho
kimeleta mabadiliko makubwa kwa wafugaji hao juu ya ufugaji wenye tija.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (wa kwanza kulia) jana tarehe 29/05/2024 akiwa na Viongozi wa Chama na Serikali wa Mkoa wa Tanga pamoja na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, amezindua Miondombinu ya majengo na vifaa vya maabara kwenye mradi wa Maziwa Faida Katika Kampasi ya TALIRI mkoani Tanga,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni