Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka kuona mabadiliko makubwa kwenye sekta ya Mifugo na Uvuvi kwa kuona vijana na akina mama wengi wanaingia kwenye sekta hizo ili kujiongezea kipato na kuongeza pato la Taifa
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara hiyo kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam Julai 07, 2023.
“Kwa maelekezo ya Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeelekezwa kuingia kwenye mpango wa BBT (Building better tomorrow) ambao tunawaandaa vijana kwa lengo la kufanya ufugaji na Uvuvi kibiashara sio tu bora kufuga, kwa wale watakaokuwa wananenepesha Ng'ombe kwa lengo la kupeleka viwandani na kuuza sambamba na watakaofuga samaki kwenye vizimba na mabwawa.” Alisema Mhe. Ulega.
Mhe. Ulega aliongeza kuwa kwa upande wa ukanda wa Pwani tunautumia ipasavyo kwa ajili ya vijana waweze kunenepesha Kaa pamoja na kufuga majongoo bahari ili waweze kujiongezea kipato chao pamoja na familia zao na kuongeza pato la Taifa.
Sambamba na hili alisema kuwa Wizara imejipanga kuhakikisha fursa za rasilimali mifugo na Uvuvi zitumike ipasavyo kwenye kuinua taifa letu
“Tumepanga kuwaondosha wafugaji na wavuvi katika zana duni na kuwapeleka katika zana za kisasa, Wizara imeanza na kuwawezesha wavuvi boti 160 za kisasa zenye GPS na zenye uwezo wa kuhifadhi tani 1 za samaki, na boti hizi zinakopeshwa kwa wavuvi bila riba, boti hizi zitawasaidia wavuvi kufika mbali Zaidi.”
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (kulia) akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Wizara hiyo mara baada ya kuwasili kwenye maonesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 07, 2023 kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ranchi za Taifa (NARCO) Prof. Peter Msofe.
Mtaalam kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Richard Mwakapuja (kushoto) akitoa elimu kuhusiana na matumizi sahihi ya chanjo zinazozalishwa na Wakala hiyo kwa Naibu Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi (kulia) wakati alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam, Julai 07,2023
Naibu Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi (kushoto) akiongea na watendaji wa Bodi ya Nyama Tanzani (TMB) wakati alipotembelea banda hiyo kwenye Maonesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 07,2023,
Mjasiriamali mdogo kutoka kiwanda cha Waasili Asilia Bw. Dedan Judcate (kulia) akielezea bidhaa za ngozi wanazotengeneza na changamoto zinazowakabili kwa Naibu Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi (kushoto) wakati alipotembelea banda lao wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 07,2023
Naibu Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi (kushoto) akitoa maelekezo kwa watendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) wakati alipotembelea banda hili kwenye maonesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 07,2023
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Daniel Mushi (kushoto) akipata maelezo kuhusiana na aina za Chanjo za Mifugo zinazozalisha Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA kutoka kwa Wataalam wa TVLA, DKt. Geofrey Omarch pamoja na Dkt. Richard Mwakapuja alipotembelea banda la TVLA lililopo Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam siku ya tarehe 07/07/2023.
Mtaalam kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA Bwana Msafiri Kaloka akitoa elimu kwa wanafunzi wa Chuo cha Kilimo cha Borigaram kilichopo Kigamboni (borigaram agriculture technical college) waliotembelea banda la TVLA kujifunza shughuri za kimaabara zinazofanya na TVLA kuhusiana na namna vimelea vya bakteria vinavyooteshwa kwa ajili ya kuweza kutambua aina ya dawa inayoweza kutibu ugonjwa pamoja na magonjwa yanayoenezwa na wadudu aina ya Ndorobo na Kupe kwa wanyama siku ya tarehe 07/07/2023 kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam.
Mtaalam kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA Bwana Shukuru Guo akitoa elimu kwa wadau wa Mifugo (watawa wa kanisa katoriki) waliotembelea banda la TVLA kuhusiana na matumizi sahihi ya chanjo za Mifugo zinazozalishwa na Wakala siku ya tarehe 07/07/2023 kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni