Afisa Utalii kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Bw. Davis Mpotwa akitoa elimu juu ya umuhimu wa kuhifadhi maeneo ya mazalia ya samaki kwa ajili ya uvuvi endelevu na utalii kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam. Julai 4,2023
Afisa Mteknolojia wa chakula kutoka Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) , Bi. Fatihiya Abdallah (kulia) akitoa elimu ya upimaji ubora wa maziwa kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya sabasaba jijini dar es salaam, julai 4, 2023
Mkufunzi kutoka Wakala wa Elimu na mafunzo ya Uvuvi (FETA) Bw. Omary Mussa (kushoto) akitoa elimu ya ufugaji jongoo bahari, mwani, ufugaji wa samaki kwenye vizimba na samaki wa mapambo kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kitaifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam Julai 4,2023
Afisa Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kanda ya mashariki, Bw. Valentino Urassa (kulia) akitoa elimu juu ya malisho na lishe ya wanyama kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam , Julai 4,2023
Mhandisi wa Kilimo na Mifugo kutoka Taasisi ya Wakala ya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) Mpwawa, Eng. Yasin Salahe (kulia) akitoa elimu ya mafunzo ya afya na uzalishaji wa mifugo kwa vijana waliomaliza kidato cha nne na cha sita, ngazi ya cheti na diploma wakati wa maonesho ya 47 kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya sabasaba jijini dar es salaam, julai 4, 2023
Mchakataji nyama kutoka Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) Ruvu, Bi. Judith Dioniz akitoa elimu ya utaalam wa nyama kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika jijini Dar es salaam, Julai 4, 2023
Afisa Mifugo Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Happiness Lyimo (kushoto) akutoa elimu kwa njia ya machapisho kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya sabasaba jijini dar es salaam, Julai 4, 2023.
Mdau wa Sekta ya Mifugo kutoka Kampuni ya Panicium Limited, Dkt. Baguma Egbert , akitoa elimu ya uhimilishaji, lishe, aina bora za nguruwe pamoja na sayansi ya ufugaji wa nguruwe, kwenye banda la Wizara ya mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam, Julai 4,2023
Mdau wa Uchakataji dagaa, mwani, unga wa dagaa na unga wa mwani kutoka Sekta ya Uvuvi Bi. Esther kunambi, kutoka Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam akieleza namna anavyochakata mazao hayo ya uvuvi kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam, Julai 4,2023
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni