Nav bar

Ijumaa, 19 Mei 2023

VIONGOZI WA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI WAFANYA KIKAO NA WAWAKILISHI WA BENKI YA NMB

 

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (katikati) akiongea wakati wa  kikao cha Watendaji wa Wizara hiyo na wawakilishi kutoka benki ya NMB makao Makuu  (hawapo pichani)  lengo likiwa ni pamoja na kuona namna benki hiyo inaweza kushirikiana na wavuvi pamoja na wafugaji kwa kuwakopesha na kupata mitaji zaidi Mei 9, 2023 jijini Dodoma.


Naibu katibu Mkuu (Mifugo), Dkt. Daniel Mushi akiongea wakati wa  kufunga kikao cha watendaji wa Wizara ya  Mifugo na Uvuvi pamoja na wawakilishi kutoka benki ya NMB Makao Makuu  (hawapo pichani) walipoenda kutembelea Wizarani hapo na kujadili namna wanaweza kutoa mikopo kwa wafugaji na wavuvi, Mei 9,2023

Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Biashara (Kilimo, Uvuvi na Miti) kutoka benki ya NMB Makao Makuu, Bw. Nsolo Mlozi akieleza namna benki na NMB ilivyodhamiria  kuwahudumia Wavuvi  na wafugaji ili nao waweze kunufaika na mikopo  wakati wa kikao kifupi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mtumba jijini Dodoma Mei 9, 2023.


Sehemu ya watendaji kutoka Wizara ya mifugo  na Uvuvi pamoja na wawakilishi kutoka benki ya NMB makao makuu, wakifuraiya jambo wakati wa kikao mtumba jijini Dodoma,  Mei 9, 2023.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni