Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Biashara kutoka NMB, Bw. Isaac Masusu (kulia) wakati akieleza kuhusu huduma za kibenki ambazo wafugaji na wavuvi wanaweza kuzitumia ili kuboresha shughuli zao. Wengine katika picha ni sehemu ya ujumbe kutoka katika benki ya NMB walipomtembelea Mhe. Ulega, Machi 23, 2023. Uongozi huo ulimueleza Mhe. Waziri kuwa wao wapo tayari kushirikiana na Wizara kuboresha shughuli za wafugaji na wavuvi.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi kutoka Benki ya NMB walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma Machi 23, 2023. Kushoto ni, Mkuu wa Idara, Huduma za Serikali, Bi. Vicky Bishubo.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe akiongea na Uongozi kutoka Benki ya NMB (hawapo pichani) walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma Machi 23, 2023. Uongozi huo ulifika ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha na kueleza kuhusu huduma za kibenki wanazozitoa ambazo miongoni mwake zina fursa kwa ajili ya wafugaji na wavuvi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi kutoka Benki ya NMB walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma Machi 23, 2023.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni