Nav bar

Ijumaa, 25 Novemba 2022

MAAFISA UGANI WAPATIWA MAFUNZO REJEA

 


Mkuu wa Idara ya Mifugo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza Dkt. Chrispine Shami akizungumza wakati akiwakaribisha maafisa ugani (hawapo pichani) kwenye mafunzo rejea yanayofanyika katika wilaya hiyo yakihusisha maafisa kutoka Kanda ya Ziwa Magharibi inayohusisha mikoa ya Kagera, Mwanza na Geita na kuandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kuwajengea uwezo, elimu na maarifa mapya. (17.11.2022)


Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti Mafunzo na Ugani kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Angelo Mwilawa akizungumza wakati wa kuanza kwa mafunzo rejea ya siku mbili kwa maafisa ugani (hawapo pichani) kutoka Kanda ya Ziwa Magharibi inayohusisha mikoa ya Kagera, Mwanza na Geita. Mafunzo hayo yanafanyika katika Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, ambapo Dk. Mwilawa amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo maafisa hao na wadau wa sekta ya mifugo elimu rejea na maarifa mapya pamoja na kuchochea ufugaji wa kisasa na biashara. (17.11.2022)


Afisa Utafiti Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Mathew Mgogo akifafanua juu ya vigezo vya kupima maafisa ugani pamoja na majukumu yao wakati wa kuanza kwa mafunzo rejea ya siku mbili kwa maafisa ugani (hawapo pichani) kutoka Kanda ya Ziwa Magharibi inayohusisha mikoa ya Kagera, Mwanza na Geita. Mafunzo hayo yanafanyika katika Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza. (17.11.2022)


Afisa Utafiti Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Grace Masolwa akielezea juu ya matumizi ya huduma za ugani kiganjani kwa kutumia simu janja wakati wa kuanza kwa mafunzo rejea ya siku mbili kwa maafisa ugani (hawapo pichani) kutoka Kanda ya Ziwa Magharibi inayohusisha mikoa ya Kagera, Mwanza na Geita. Mafunzo hayo yanafanyika katika Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza. (17.11.2022)


Baadhi ya maafisa ugani kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa wakiwa kwenye mafunzo rejea yanayofanyika katika wilaya hiyo yakihusisha maafisa hao kutoka Kanda ya Ziwa Magharibi inayohusisha mikoa ya Kagera, Mwanza na Geita na kuandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kuwajengea uwezo, elimu na maarifa mapya. (17.11.2022)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni