Nav bar

Alhamisi, 17 Novemba 2022

DKT. TAMATAMAH AFANYA MAZUNGUMZO NA MRATIBU WA MRADI WA KUHAMASISHA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI KIKANDA NA UKUZAJI VIUMBE MAJI ENDELEVU

 


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Dkt. Alexander Keffi (kulia) ambaye ni Mratibu wa Mradi wa  Kuhamasisha  Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Kikanda na Ukuzaji Viumbe Maji Endelevu (PROFISHBLUE) wakati alipofika kwenye Ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali - Mtumba Jijini Dodoma. Lengo la ujio wake ni kutambulisha Mradi huo ambao unaratibiwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Wengine katika picha ni viongozi na wataalam kutoka Sekta ya Uvuvi. (09.11.2022)


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mratibu wa Mradi wa Kuhamasisha Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Kikanda na Ukuzaji wa Viumbe Maji Endelevu (PROFISHBLUE), Dkt. Allexander Keffi (wa tatu kutoka kulia) mara baada ya kumalizika kwa kikao kifupi cha kutambulisha Mradi huo ambao upo chini ya Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADC). Wengine ni viongozi na wataalam kutoka Sekta ya Uvuvi. Kikao hicho kimefanyika kwenye Ofisi za Wizara zilizopo kwenye Mji wa Serikali - Mtumba Jijini Dodoma. (09.11.2022)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni