Serikali imewataka wakaguzi wa maeneo ya malisho na rasilimali za vyakula vya mifugo kuhakikisha mifugo inapatiwa vyakula vyenye ubora na stahiki ili kuondokana na madhara ya sumukuvu yanayoweza kuwaathiri walaji wa nyama, mayai, maziwa na bidhaa nyingine za mazao ya mifugo.
Rai hiyo imetolewa na Kaimu
Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Bw. Peter Nyakigera wakati akifungua mafunzo ya
wakaguzi wa maeneo ya malisho na rasilimali za vyakula vya mifugo yaliyofanyika
leo Agosti 12, 2021 katika ukumbi wa siasa ni kilimo Mkoani Iringa.
Nyakigera alisema kuwa
mafunzo hayo ni muhimu sana kwa wakaguzi walio kwenye mamlaka za serikali za
mitaa kwa vile yatasaidia kutatua changamoto ya ubora na viwango hafifu vya
vyakula vya mifugo vinavyotumiwa na wafugaji walio wengi ambapo hata vifo vya
baadhi ya mifugo vimesabishwa na kutumia baadhi ya rasilimali za vyakula vyenye
sumukuvu.
“Tanzania ni nchi ya pili
kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo Afrika ikiwa na ng’ombe milioni 33.4, mbuzi
milioni 21.29, kondoo milioni 5.65, kuku milioni 83.28 ambapo kwa mwaka
2019/2020 zilizalishwa hadi lita bilioni 3.01 za maziwa, tani 701,679 za nyama
na mayai bilioni 4.05 hivyo uzalisaji wa mazao haya kwa kiasi kikubwa
unategemea upatikanaji wa uhakika wa rasilimali za vyakula vya mifugo vyenye
ubora na viwango stahiki” alisema Bw. Nyakigera.
Nyakigera alisema kuwa
wakaguzi hao wanawajibu mkubwa wa kulinda afya za walaji na mifugo yenyewe kwa
kusimamia sheria na kanuni ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kutosha kwa wadau
kwenye mnyororo wa thamani kwenye tasnia ya vyakula vya mifugo.
Aliongeza kuwa elimu ya ufugaji wenye tija inayoendelea
kutolewa imeongeza hamasa kwa wafugaji
hivyo ni muhimu kupatikana kwa
vyakula vyenye ubora na viwango hususani
kwa ng’ombe na kuku.
“Kuwepo kwa vyakula vyenye
ubora kutapuguza malalamiko ya ukuaji hafifu uliobainika kwa kuwa wafugaji hutumia
takribani asilimia 60 ya gharama zote za uzalishaji kwenye vyakula, hivyo
uzalishaji wenye tija hutegemea sana uwepo wa viini lishe vyote muhimu kwenye
vyakula hivyo” amemalizia Nyakigera.
Kwa upande wake Kaimu
Mkurugenzi wa Rasilimali za vyakula vya mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na
Uvuvi, Bw. Rogers Shengoto alisema mafunzo hayo ni moja ya utekelezaji wa
majukumu yaliyopangwa na Idara hiyo lengo likiwa ni kuhakikisha changamoto za
ubora wa vyakula vya mifugo vinavyozalishwa na vinavyotumiwa na wafugaji nchini
vinakuwa vimezingatia kanuni bora, sheria na taratibu zote ambazo zinatakiwa.
"Tunataka kuhakikisha
changamoto za ubora kwa malalamiko ya ukuaji wa wanyama na uzalishaji hafifu
unapungua kwa wazalishaji wa Mifugo. Amesema Bw. Shengoto.
Naye Mkaguzi wa maeneo ya
malisho na Rasilimali za vyakula vya mifugo kutoka Mkoa wa Babati, Bw. Mayanzi
Bubinza ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa mafunzo kwa wafugaji na
wataalam nchini.
Kaimu
Mkurugenzi wa Rasilimali za vyakula vya mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na
Uvuvi, Bw. Rogers Shengoto (wa pili kutoka kulia) akimueleza machache Kaimu
Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji Mkoa wa Iringa Bw. Peter
Nyakigera (kushoto) kabla ya ufunguzi wa mafunzo kwa wakaguzi wa maeneo ya
malisho na Rasilimali za vyakula vya mifugo nje ya ukumbi wa siasa ni kilimo
halmashauri ya wilaya ya Iringa Mkoani
Iringa Agust 12, 2021.
Kaimu
Mkurugenzi wa Rasilimali za vyakula vya
mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi , Bw. Rogers Shengoto, akimkaribisha mgeni rasmi (hayupo pichani)
Ili kuweza kufungua mafunzo ya wakaguzi wa maeneo ya malisho na Rasilimali za
vyakula vya mifugo kwenye ukumbi wa siasa ni Kilimo halmashauri ya wilaya ya
Iringa Mkoani Iringa Agosti 12, 2021.
Baadhi
ya wataalam wakitoa wafunzo kwa wakaguzi wa maeneo ya malisho na Rasilimali za
vyakula vya mifugo kwenye ukumbi wa siasa ni kilimo Mkoani Iringa Agosti 12,
2021.
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo ya wakaguzi wa maeneo ya malisho na Rasilimali za vyakula
vya mifugo yaliyofanyika Agosti 12, 2021
kwenye ukumbi wa Siasa ni kilimo Mkoani Iringa.
Kaimu
Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji (wa tatu kutoka kulia),
Bw. Peter Nyakigera akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalam wa Mifugo na wakaguzi kutoka ngazi
za Wizara na Mikoa mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya wakaguzi wa maeneo ya
malisho na Rasilimali za vyakula vya mifugo kwenye ukumbi wa Siasa ni kilimo Mkoani Iringa. (12/08/2021.)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni