Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akiongea na
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo (Zanzibar), Dkt. Soud Hassan
alipomtembelea Waziri huyo Ofisini kwake. Prof. Ole Gabriel alifanya
ziara Visiwani Zanzibar Agosti 2, 2021 kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano
baina ya Sekta ya Mifugo, Tanzania bara na Sekta ya Mifugo, Zanzibar, pia
kufanya uhamasishaji wa ufugaji wa kisasa Visiwani humo.
Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akikagua moja kati ya aina
mbalimbali za malisho ya mifugo zinazofanyiwa Utafiti na Taasisi ya
Utafiti wa Mifugo, Zanzibar (ZALIRI) alipotembelea taasisi hiyo iliyopo
Visiwani Zanzibar Agosti 2, 2021.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi
(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (wa kwanza kushoto) akiongea na Viongozi
wa Kiwanda cha kuzalisha maziwa cha Azam Kilichopo Fumba, Visiwani Zanzibar.
Prof. Ole Gabriel alifanya ziara katika Kiwanda hicho Agosti 2, 2021 kwa
lengo la kukagua maendeleo yake ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka
kuendelee kuzalisha maziwa kwa kiwango kilichokusudiwa huku akiwaeleza
kuwa Serikali ipo pamoja nao. Katikati ni Meneja wa Kiwanda hicho, Adilson
Fagundes na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Udhibiti Ubora wa bidhaa katika Kiwanda
hicho, Tumaini Fredrick.
Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (watatu kutoka kushoto)
akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na
Mifugo, Zanzibar, Dkt. Soud Hassan (katikati). Prof. Ole Gabriel alimtembelea
Waziri huyo Ofisini kwake, Visiwani Zanzibar Agosti 2, 2021.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni